Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 39 Water and Irrigation Wizara ya Maji 468 2026-05-29

Name

John Francisco Nzilanyingi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyamagana

Primary Question

MHE. SILVERY L. SALVATORY K.n.y. MHE. JOHN F. NZILANYINGI aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa matenki ya maji ya Nyamazobe, Buhongwa na Fumagila ili kuongeza upatikanaji wa maji Jiji la Mwanza?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa John Francisco Nzilanyingi, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekamilisha ujenzi wa chanzo cha maji cha Butimba kupitia maji ya Ziwa Victoria ambacho kina uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 48 kwa siku. Aidha, utekelezaji wa mradi wa kusambaza maji unaendelea kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa zaidi ya wakazi 450,000 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza na maeneo jirani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huo unahusisha ujenzi wa vituo vitatu vya kusukuma maji katika maeneo ya Butimba na Sahwa, ujenzi wa matenki matano yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 31 katika maeneo ya Buhongwa, Fumagila, Nyamazobe, Kisesa na Usagara sanjari na ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 40.5. Utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa 53% na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2026 kwa mujibu wa mkataba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutoa kipaumbele cha kupeleka fedha za utekelezaji wa mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati na ubora stahiki. Ahsante.