Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Silvery Luboja Salvatory
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Primary Question
MHE. SILVERY L. SALVATORY K.n.y. MHE. JOHN F. NZILANYINGI aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa matenki ya maji ya Nyamazobe, Buhongwa na Fumagila ili kuongeza upatikanaji wa maji Jiji la Mwanza?
Supplementary Question 1
MHE. SILVERY L. SALVATORY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na kwa niaba ya Mheshimiwa John Francisco Nzilanyingi, ninayo maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; baada ya ujenzi wa matenki kukamilika Serikali imejipangaje ili kuhakikisha kazi ya usambazaji maji kwenye mitaa itafanyika kwa haraka?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ni nini mpango wa Serikali kufikisha huduma ya maji kwenye maeneo ambayo yamekuwa na changamoto sugu kwenye upatikanaji wa maji kama vile Kata ya Mahina na maeneo mengine ya pembezoni yakiwemo ya Jimbo langu la Misungwi hususan, Usagara, Mwasonge, Mayolwa pamoja na Chole?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa maswali ya nyongeza.
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa ya John Francisco Nzilanyingi, Mbunge wa Nyamagana yaliyoulizwa na Mheshimiwa Silvery, Mbunge wa Misungwi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu ni kweli ni mradi mkubwa na wa kimkakati na ni uwekezaji na ni mapenzi makubwa ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wa Jiji la Nyamagana. Hii ni kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Mheshimiwa Mbunge wa Nyamagana kwa kuendelea kuwa sauti yao katika kuhakikisha kwamba upatikanaji wa maji unaendelea kuwa endelevu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa mradi huu unaendelea na tunao mpango unapokamilika kama ambavyo nimesema kwa jibu la msingi utakamilika Disemba, 2026 baada ya hapo tutaanza kuhakikisha tunasambaza maji katika maeneo ya pembezoni, lakini pia kuna maeneo ya miinuko ambayo jiografia yake ina changamoto tutahakikisha maji yanafika katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ni kuhusiana na maeneo ya Mahina kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameongelea. Upande wa Mahina mradi huu wa kwanza unapokamilika hautakuwa sehemu ya kupeleka maji katika maeneo ya Mahina.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahina pamoja na Kishili na Igoma kwa sasa bado wanapata maji kwa mgao. Mheshimiwa Rais ameridhia kupeleka shilingi bilioni nane specifically kwa ajili ya maeneo haya ya Mahina, Kishili pamoja na Igoma ili wananchi wa Jiji la Mwanza waweze kuondokana na mgao ambao unapitia kwa sasa. Huu utekelezaji uko katika hatua za mwisho na ninaamini kwamba utakapokamilika zaidi ya wananchi 45,000 watanufaika na mradi huu. Ahsante sana.
Name
Arif Suleiman Premji
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtwara Vijijini
Primary Question
MHE. SILVERY L. SALVATORY K.n.y. MHE. JOHN F. NZILANYINGI aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa matenki ya maji ya Nyamazobe, Buhongwa na Fumagila ili kuongeza upatikanaji wa maji Jiji la Mwanza?
Supplementary Question 2
MHE. ARIF S. PREMJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Jimbo la Mtwara Vijijini, Kata ya Dihimba inahitaji suluhisho la haraka. Kisima kilichochimbwa cha maji mwaka 1989 kimeharibika na wananchi zaidi ya 4,606 wanapitia changamoto hiyo ya maji. Ipi kauli ya Serikali ili kutatua hiyo changamoto kwa haraka? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge. Kwanza, kabisa ni mdau wa sekta ya maji. Pili, ametumia juhudi zake binafsi kuchimba visima ndani ya jimbo lake, lakini pamoja na hilo ameendelea kutupatia ushirikiano kwenye namna ya kutatua changamoto katika visima ambavyo ni kongwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe hofu Serikali kwa kushirikiana na Mheshimiwa Mbunge tutaenda kuhakikisha tunachukua hatua stahiki ili kuweza kutatua changamoto ambayo imejitokeza katika jimbo lako Mheshimiwa Mbunge. Ahsante sana.
Name
Emmanuel Peter Cherehani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ushetu
Primary Question
MHE. SILVERY L. SALVATORY K.n.y. MHE. JOHN F. NZILANYINGI aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa matenki ya maji ya Nyamazobe, Buhongwa na Fumagila ili kuongeza upatikanaji wa maji Jiji la Mwanza?
Supplementary Question 3
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Kinamapula, Kata ya Uyogo, Ulewe na Kata ya Mapamba ni kata ambazo hazina mradi kabisa wa maji, lakini pia na watafiti wamefanya chini ya ardhi hakuna maji. Hata shule za msingi na sekondari wanafunzi wale wanateseka sana. Ni nini mkakati wa dharura wa Serikali kusaidia eneo hili?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Cherehani, Mbunge wa Ushetu kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nimpongeze sana kaka yangu kwa kazi nzuri anayoifanya, lakini pia tunao mradi mkubwa katika Jimbo lake la Ushetu ambapo Mheshimiwa Waziri wa Maji na Mheshimiwa Waziri Mkuu wakati akiwa Waziri wa Fedha walienda kusaini ndani ya jimbo lake na huo mradi tunaamini kwamba unaenda kutatua changamoto nyingi, lakini tunatambua kwamba ukubwa wa tatizo bado unahitaji jicho la Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwahidi Mheshimiwa Mbunge tutaenda kuhakikisha tunafanya tathmini na kujiridhisha katika maeneo ambayo bado hayatopitiwa na miradi inayoendelea ili tuweze kufanya usanifu na kufikisha huduma ya maji safi na salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunaendelea kuzingatia na kuchukua hatua kutokana na maelekezo ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ya kuhakikisha shule, zahanati na taasisi zingine za umma zinapatiwa huduma ya maji safi na salama ili kutosababisha magonjwa ambayo ni ya mlipuko. Ahsante sana.
Name
Hawa Subira Mwaifunga
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SILVERY L. SALVATORY K.n.y. MHE. JOHN F. NZILANYINGI aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa matenki ya maji ya Nyamazobe, Buhongwa na Fumagila ili kuongeza upatikanaji wa maji Jiji la Mwanza?
Supplementary Question 4
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kuniona. Maji ya Ziwa Victoria yameshafika katika Jimbo la Tabora Mjini na tenki la Itumba linapokea maji kutoka Ziwa Victoria na kufika pale kwa ajili ya kusambaza kwa ajili ya wananchi wa Tabora.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa miundombinu ya mabomba kutoka Bwawa la Igombe kupeleka maji kwenye tenki la Itumba ili changamoto yoyote inapotokea katika Ziwa Victoria basi maji yale yaweze kusaidia wananchi kupata maji kwa urahisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nini mpango wa Serikali kupeleka kiasi cha shilingi bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa mabomba haya ili tuweze kupata maji wakati wote hata kama kunapatikana changamoto katika mitambo ya Ziwa Victoria?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hawa Mwaifunga, Mbunge wa Tabora Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo ambalo Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi imetekelezwa kwa kishindo ni katika Jimbo la Tabora Mjini. Upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama ndani ya Tabora Mjini ni zaidi ya 98%, lakini kinachotakiwa hapa, Mheshimiwa Mbunge anachohitaji, ni resilience au backup, in case linatokea jambo ambalo maji ya Ziwa Victoria yana changamoto, basi maji ya kutoka Igombe yaweze kutumika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakutoa hofu Mheshimiwa Hawa, tumepokea kwa sababu wananchi wa Tabora Mjini ni wa thamani sana kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tutahakikisha fedha hizo tunazipeleka, tukaweke mabomba hayo ili yaweze kuhakikisha kwamba yanatengeneza backup ya kutosha kwa ajili ya maji ya wananchi wa Tabora Mjini. Ahsante sana.