Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 39 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 469 2026-05-29

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza: -

Je, Serikali inatoa elimu bure au inatoa elimu bila ada?

Name

Prof. Adolf Faustine Mkenda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rombo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) K.n.y. WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwita Mwikwabe Waitara, Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kutekeleza sera ya utoaji wa elimu-msingi bila mzazi/mlezi kuchangia ada. Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali ilitoa Waraka wa Elimu Na. 03 wa mwaka 2016 kuhusu utekelezaji wa elimu-msingi bila malipo ambapo umebainisha majukumu ya kila mdau na kuweka utaratibu wa namna wanavyoweza kuchangia michango mbalimbali katika kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu katika maeneo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 hadi 2025/2026, Serikali imetoa jumla ya shilingi 1,394,885,918,000 kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa shule. Kati ya fedha hizo shilingi 488,190,858,000 zimetolewa kwa shule za msingi na shilingi 906,695,060,000 zimetolewa kwa shule za sekondari. Utoaji wa fedha hizi umeendelea kuimarisha utekelezaji wa Sera ya Elimu Bila Malipo pamoja na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kusisitiza wadau wote wa elimu kuzingatia taratibu, kanuni na miongozo iliyowekwa ili kuimarisha mazingira bora ya ufundishaji na ujifunzaji, kuongeza upatikanaji wa elimu na kuendelea kuboresha ubora wa elimu nchini. Ahsante.