Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 39 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 470 2026-05-29

Name

Amosy William Maganga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. ENG. AMOSY W. MAGANGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itatoa mapori ya akiba kwa ajili ya ufugaji, kilimo na urinaji asali Sikonge?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Amosy William Maganga, Mbunge wa Jimbo la Sikonge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inasimamia maeneo ya mapori ya akiba kwa mujibu wa Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori nchini, Sura 283. Sheria hiyo imeweka bayana shughuli mbalimbali zinazoruhusiwa na zisizoruhusiwa ndani ya maeneo ya hifadhi kwa kuzingatia malengo na umuhimu wa kutenga maeneo hayo kwa shughuli za uhifadhi. Kwa mujibu wa sheria hiyo, shughuli za kibinadamu, ikiwemo kilimo na mifugo, haziruhusiwi kufanyika ndani ya mapori ya akiba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kutekeleza dhana ya ushirikishwaji wa jamii katika kuhifadhi rasilimali za wanyamapori na mazingira yake nchini kwa kuruhusu wananchi kutekeleza shughuli za kiuchumi, ikiwemo uvuvi na ufugaji nyuki ambazo ni rafiki katika baadhi ya mapori ya akiba. Lengo la kuanzisha shughuli hizo ni kuwawezesha wananchi kupata fursa ya kujipatia kipato na kujikimu kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mathalani, katika kipindi cha mwezi Julai hadi Disemba, 2025, jumla ya vibali 3,814 vya ufugaji nyuki vilitolewa kwa wananchi 3,354 kutoka katika Wilaya za Mlele, Sikonge, Kibondo, Kasulu na Kakonko. Vibali hivyo vilitolewa katika Mapori ya Akiba Moyowosi (2,625), Ugalla (478), Rukwa (117) na Inyonga (136) kutokana na mahitaji ya wananchi wa eneo husika.