Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Amosy William Maganga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Sikonge
Primary Question
MHE. ENG. AMOSY W. MAGANGA aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa mapori ya akiba kwa ajili ya ufugaji, kilimo na urinaji asali Sikonge?
Supplementary Question 1
MHE. ENG. AMOSY W. MAGANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, pamoja na majibu ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2021 Tume ya Mawaziri Wanane ilizunguka katika nchi hii ili kubaini changamoto na migogoro, hususan katika vijiji ambavyo vinapakana na misitu ya akiba. Wilayani Sikonge tunashukuru tume hiyo ilifika na kwamba katika Wilaya yetu ya Sikonge waliweza kutoa kiasi cha hekta 5,000 ili ziweze kugawanywa kwa wananchi wa Nyahua, pamoja na Kipili, lakini mpaka tunavyoongea hivi sasa hilo eneo bado halijagawiwa kwa sababu ya ukosefu wa takribani shilingi milioni 500, ili kutekeleza mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Je, Serikali haioni sasa kuna sababu ya kutoa hizo shilingi milioni 500 ili hawa wananchi waweze kugawiwa maeneo na kuondoa hizo changamoto zilizopo katika maeneo hayo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile swali la pili; hii tume ilienda muda mrefu kidogo, takribani miaka mitano na mpaka hivi sasa kilio cha wananchi kutafuta maeneo kimekuwa ni kikubwa sana.
Je, Mheshimiwa Naibu Waziri, haoni kwamba kuna sababu ya kuongozana pamoja na mimi ili kusudi aweze kuwasikiliza hawa wananchi na hatimaye aweze kutoa ushauri mzuri kwa Serikali, ili hawa wananchi waweze kuongezewa maeneo pamoja na maeneo ambayo tume hiyo haikuweza kufika?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nampongeza Mheshimiwa Amosy Maganga, Mbunge wa Sikonge kwa maswali mawili ya nyongeza yenye faida kwa wananchi wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli mwaka 2021 Tume ya Mawaziri Nane ilifika katika eneo la Sikonge na mimi nilikuwa ni sehemu ya hiyo tume, nilifika eneo hilo. Ni kweli, tulitenga hilo eneo, lakini moja ya maelekezo ambayo tulitoa ni kwamba lazima eneo linalotolewa lipangwe na kuwe na matumizi sahihi ya eneo husika na halmashauri iliji-commit kutoa shilingi milioni 500, lakini kutokana na changamoto hiyo namthibitishia tu kwamba Serikali itakaa pamoja na halmashauri na Wizara ya Ardhi na kutafuta namna bora ya kuweza kupata ufumbuzi wa jambo hilo. Kwa hiyo, tutakaa pamoja as a team kabla hatujatoa jibu la mwisho, ili tuweze kutoka vizuri katika jambo hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kutembelea eneo hilo, jana Waziri wa Ardhi hapa wakati anahutubia Bunge, alisema moja ya eneo ambalo anakwenda kulifanyia kazi na ametengeneza mpango, ni ile Tume ya Mawaziri Wanane kumalizia ile kazi ambayo ilikuwa imebaki. Kinachotakiwa hapa ni sisi tu Wabunge tupitishe bajeti yake, ili ule mpango ambao Waziri ameuainisha wa Mawaziri Nane tuweze kwenda huko. Kwa hiyo, ni tofauti na kumtaka Naibu Waziri peke yake, tume ifike katika eneo hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti hii ndiyo itakayotusaidia kufika katika eneo hilo, ukiacha Waziri kufika, lakini Mawaziri Nane na wenyewe watafika baada bajeti hii kuweza kupitishwa. Kwa hiyo, namthibitishia Mheshimiwa Mbunge, tume itafika, lakini na Naibu Waziri au Waziri husika atafika katika eneo lako. Ahsante sana.
Name
Janeth Elias Mahawanga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ENG. AMOSY W. MAGANGA aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa mapori ya akiba kwa ajili ya ufugaji, kilimo na urinaji asali Sikonge?
Supplementary Question 2
MHE. JANETH E. MAHAWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nakushukuru kwa nafasi. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza maeneo ya uzalishaji bila kuharibu mazingira na Hifadhi za Taifa?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ninafikiri mpango wa kuongeza maeneo ya uwekezaji ni sehemu ambayo ukiangalia wakati wa hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, aliainisha namna bora ya kuongeza maeneo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya maeneo ambayo tunakwenda kuongeza, kutenga maeneo, kwa ajili ya kilimo, mifugo na uvuvi ni sehemu ya hayo mambo. Wizara ya Ardhi inafanya jukumu hilo la kuhakikisha kwamba wawekezaji wanapokuja hapa nchini, pamoja na wawekezaji wa ndani wanapata maeneo hayo bila usumbufu wowote na wanawekeza. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved