Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 47 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 555 | 2026-06-10 |
Name
Edibily Kinyoma Kazala
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kasulu Vijijini
Primary Question
MHE. EDIBILY K. KINYOMA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Kata za Asante Nyerere na Kata ya Shunguliba kwa kiwango cha changarawe?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA
SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Edibily Kazala Kinyoma, Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali imefanya matengenezo ya kawaida kwenye Barabara ya Uvinza Junction - Asante Nyerere kwa kuchonga kilometa 11.46 ambapo pia kiwango cha Changarawe kilometa 2.5 kimewekwa kwa gharama ya shilingi milioni 68.41. Aidha, katika mpango wa bajeti ya mwaka 2026/2027, barabara itafanyiwa matengenezo
kwa gharama ya shilingi milioni 16 kwa ajili ya kuweka changarawe kilometa moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Asante Nyerere – Mwitiri kwa mwaka wa fedha 2025/2026 imechongwa kilometa mbili na itawekewa changarawe kilometa mbili, matengenezo yote yatagharimu shilingi milioni 32. Aidha, kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imefanya matengenezo ya kawaida katika
Barabara ya Shunguliba – Rungwe Mpya katika Kata ya Shunguliba kwa kuchonga kilometa tisa na itawekwa Changarawe kilometa 3 kwa gharama ya shilingi milioni 81.94
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali itafanya matengenezo ya kawaida kwa kuweka changarawe barabara sita za Kata ya Shunguliba kwa gharama ya shilingi milioni 92.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuzijenga, kuzikarabati na kuzifanyia matengenezo barabara zote za mjini na vijijini kote nchini ikwemo barabara za Wilaya ya Kasulu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved