Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Edibily Kinyoma Kazala
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kasulu Vijijini
Primary Question
MHE. EDIBILY K. KINYOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Kata za Asante Nyerere na Kata ya Shunguliba kwa kiwango cha changarawe?
Supplementary Question 1
MHE. EDIBILY K. KINYOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na ninakushukuru. Kwanza, nimshukuru Waziri, lakini pia niishukuru Serikali kwa kuniona kwa kuniletea kile kipande cha barabara kwa kujenga kwa kiwango cha changarawe, lakini nilitaka niulize maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kipande cha
kutoka Asante Nyerere kwenda Mwitiri mpaka Kanenge na kutoka Mwitiri mpaka Kagege vile vipande havina barabara kabisa na inahitaji kama shilingi 310,000,000 tu kidogo na ni kilometa 10 tu, na wananchi walishaanza kuchonga. Je, Serikali haioni iko haja ya kuunga jitihada za wananchi kwa kuzichonga vizuri zile barabara na kuziwekea changarawe?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Kata ya Shunguliba ile kata haina mtandao kabisa wa barabara wa kuunganisha vijiji vyake vitatu, haina kabisa na wananchi wanakosa huduma, barabara haipitiki mpaka magari ya kuchonga na kuchimba visima yalishindwa kupita. Kwa hiyo, ...
MWENYEKITI: Swali Mheshimiwa.
MHE. EDIBILY K. KINYOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali haioni iko haja ya kuweka mpango wa dharura kuzichonga zile barabara angalau zipitike kutoka Shunguliba kwenda Kazage, Kazage kwenda Malalo? Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na nimpongeze sana Mheshimiwa Edibily Kazala Kinyoma, Mbunge wa Kasulu Vijijini kwa ufuatiliaji wake wa mara kwa mara kuhusiana na miradi ya barabara jimboni kwake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie
Mheshimiwa Mbunge kwamba tunafahamu ziko barabara katika Jimbo la Kasulu Vijijini ambazo zimeharibika kufuatia mvua nyingi zilizonyesha, lakini zipo ambazo hazijakarabatiwa kwa muda mrefu na ndio maana katika jibu langu la msingi tunazo bajeti za
kwenda kutengeneza barabara hizi; Barabara ya Asante Nyerere lakini na barabara hii ya maeneo ya Kata ya Shunguliba. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba vipande vya barabara hivyo kilometa 10 ambavyo wananchi kwa nguvu zao wamefungua barabara zile kwanza, nikupongeze
Mheshimiwa Mbunge na wananchi kwa kuthubutu kuanza ufungua barabara hizo, lakini nikuhakikishie kwamba Serikali ina utaratibu mzuri, kwanza tunazitambua barabara na kuzisajili kupitia mtandao wa TARURA.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nitumie nafasi hii
nimwelekeze Meneja wa TARURA Wilaya ya Kasulu na Mkoa wa Kigoma wapitie barabara hizo ambazo ndio mpya zimefunguliwa na wananchi na kuona kama zinakidhi vigezo vya kusajiliwa kuwa sehemu ya mtandao wa TARURA wafanye hivyo ili barabara hizo
zitambuliwe rasmi na kuanza kutengewa fedha ili Serikali iweze kupeleka fedha kwa ajili ya matengenezo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili, kuhusiana na barabara za Kata za Shunguliba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tayari tunaendelea na kutangaza zabuni kwa ajili ya barabara zote zilizoathirika hasa barabara zile muhimu na tutahakikisha barabara za Kata ya Shunguliba zinapewa kipaumbele. (Makofi)
Name
Mohamed Mussa Utaly
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lindi Mjini
Primary Question
MHE. EDIBILY K. KINYOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Kata za Asante Nyerere na Kata ya Shunguliba kwa kiwango cha changarawe?
Supplementary Question 2
MHE. MOHAMED M. UTALY: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninashukuru sana kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo la Lindi ipo barabara ambayo inajengwa kupitia Mradi wa TACTIC, lakini mkandarasi ameshapewa mkataba, lakini anasuasua mpaka sasa katika suala la ujenzi wa barabara hii na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amekutana na mkandarasi huyu lakini bado anaonekana hatakelezi majukumu yake ipasavyo.
Je, Mheshimiwa Naibu Waziri, upo tayari kuambatana nami sako kwa bato kwenda kuonana na kuzungumza naye ili aweze kurekebisha mwenendo wake na barabara hii ijengwe kwa manufaa ya wananchi wa Lindi? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Manispaa ya Lindi ni moja ya halmashauri ambazo zina Miradi ya TACTIC na ikiwemo ujenzi wa barabara za lami na ni kweli kama alivyosema Mheshimiwa Utaly, Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwamba tulishapata
mkandarasi na amekuwa site.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nipokee hoja kwamba, mradi huo hauendi kwa kasi inayotakiwa na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwanza, leo tutawasiliana na Meneja wa TARURA wa Mkoa wa Lindi ili watupe taarifa rasmi kwa nini mkandarasi huyo hafanyi kazi kwa kasi inayotakiwa na ikiwa kuna
vifungu vya kimkataba ambavyo vimekiukwa tutachukua hatua kwa mujibu wa sheria.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, nitumie nafasi hii nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kwamba barabara zetu zote za Mradi wa TACTIC zinakamilika na barabara hiyo itakamilika.
Name
Jackson Gedion Kiswaga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalenga
Primary Question
MHE. EDIBILY K. KINYOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Kata za Asante Nyerere na Kata ya Shunguliba kwa kiwango cha changarawe?
Supplementary Question 3
MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Kwanza ninaishukuru Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, tumekuwa na barabara ambayo imekuwa ikisumbua kwa miaka miwili kutoka Magunga – Wasa na sasa mkataba wake
umesainiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali, tunayo barabara ya kutoka Mwimbi – Ulete – Isupilo, hii barabara imeharibika sana kutokana na mvua; je, ni lini sasa Serikali itatupandishia hadhi barabara hii ili iweze kujengwa kwa kiwango cha changarawe na ili iweze
kudumu kwa muda mrefu? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimthibitishie Mheshimiwa Kiswaga, Mbunge
wa Jimbo la Kalenga na bahati nzuri miezi miwili iliyopita nilifanya ziara katika jimbo lake na ni kweli tuliona baadhi ya barabara ikiwemo barabara aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge, ziliathirika sana na mvua zilizomaliza kunyesha msimu uliopita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie
Mheshimiwa Mbunge kwamba tumeshatoa maelekezo kwa Mameneja wa TARURA wa Wilaya na Mikoa kuainisha barabara zote ambazo ziko maeneo hatarishi zaidi na zinaathirika zaidi na mvua ili tuzibadilishe barabara hizo kwenda kiwango cha changarawe, lakini tujenge mifereji, madaraja na makalvati ya kutosha ili kuhakikisha kwamba barabara hizo zinadumu kwa
muda mrefu.
Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Kiswaga na wananchi wa Jimbo la Kalenga kwamba barabara hiyo tutaipa kipaumbele kuhakikisha kwamba tunaiboresha zaidi.
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. EDIBILY K. KINYOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Kata za Asante Nyerere na Kata ya Shunguliba kwa kiwango cha changarawe?
Supplementary Question 4
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Barabara ya Chimbuya – Ukwile – Chizumbi – Msamba One na Barabara ya Vwawa – Gereza la Vwawa – Old Vwawa zimekuwa hazipitiki kwa muda mrefu sana. Ni upi mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kwamba hizi barabara zinatengenezwa kwa wakati? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa Serikali ni kuhakikisha kwamba barabara zote ambazo hazipitiki na barabara muhimu zaidi katika maeneo
yetu ambazo zinapitiwa na wananchi wengi kwa shughuli za usafirishaji zinapewa kipaumbele, kwanza kwenye bajeti zetu, lakini pili kwenye matengenezo ya dharura.
Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Hasunga, Mbunge wa Jimbo la Vwawa kwamba barabara ulizozitaja tutazipa kipaumbe, kwanza kwenye 60% ambayo tunatangaza, lakini pia kwenye matengenezo ya dharura tutahakikisha kwamba tunazipa kipaumbele kwa ajili ya kutengeneza barabara
hizo ziweze kupitika vizuri. (Makofi)
Name
Edefonce Joackim Canoni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Primary Question
MHE. EDIBILY K. KINYOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Kata za Asante Nyerere na Kata ya Shunguliba kwa kiwango cha changarawe?
Supplementary Question 5
MHE. EDIFONSI J. KANONI: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninashukuru sana kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Kalambo katika Kata ya Mpombwe Kijiji cha Chipwa, kutoka makao makuu ya kata kwenye Kijiji cha Chipwa ambacho kipo mpakani mwa Zambia na Tanzania ni kilometa 6.8 hawajawahi kuwa na barabara toka kupata uhuru, lakini kwenye ilani ya mkoa ipo kwenye bajeti ya
kujengewa barabara kwa kiwango cha mawe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia kuna maporomoko ya utalii ambayo ni ya historia, ni ya pili Afrika yenye urefu wa meta 335. Nini mpango wa Serikali kujenga barabara hii ambayo wananchi wanapata shida kutoka kijijini kwenda makao makuu, hadi watembee kwa mguu ili kwenda kupata huduma za kimsingi? Mpango wa Serikali kupanga bajeti ili kuweza kuijenga barabara hii kwa kiwango cha changarawe.
Mheshimiwa Waziri ninaomba majibu. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ni kweli kwamba katika Jimbo la Kalambo tunayo Maporomoko ya Kalambo (Kalambo Falls) ambayo mimi nilipata bahati ya kuyatembelea, ni maporomoko
mazuri sana. Kwa hiyo, ninawashauri Waheshimiwa Wabunge wakipata nafasi na Watanzania kwa ujumla kuyatembelea maporomoko yale mazuri sana na marefu ya pili katika Bara la Afrika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba barabara ile
inahitaji matengenezo na ninakubaliana na Mheshimiwa Kanoni, Mbunge wa jimbo hilo. Nitumie nafasi hii kwa sababu barabara ile kwa maelezo ya Mheshimiwa Mbunge bado haijasajiliwa TARURA. Kwa hiyo, Meneja wa TARURA wa Mkoa wa Rukwa na Wilaya ya Kalambo wafike katika barabara hiyo waifanyie tathmini, na kutokana na umuhimu wake kwa shughuli za kitalii na shughuli za usafiri kwa wananchi, waiingize kwenye utaratibu wa kuisajili kwenye mtandao wa TARURA ili tuanze kuitengea bajeti kwa ajili ya matengenezo.
Name
Morris Joseph Makoi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Mjini
Primary Question
MHE. EDIBILY K. KINYOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Kata za Asante Nyerere na Kata ya Shunguliba kwa kiwango cha changarawe?
Supplementary Question 6
MHE. MORRIS J. MAKOI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kupata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo la Moshi Vijijini Kata ya Mbokomu, Barabara ya Kiboriloni – Mbokomu – Mti Mrefu ina kilometa 13.94. Serikali imekubali kujenga meta 200 kwa awamu, lakini wananchi wa Mbokomu kwa sasa wamehamasishana wanachanga fedha takribani shilingi milioni 400 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa barabara hii ya lami.
Je, Serikali iko tayari kuungana nao katika jitihada hizi
kuhakikisha kwamba hiyo barabara inajengwa zaidi ya hizo meta 200?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Moshi Vijijini na hususan katika eneo hilo la
Mbokomu na mimi ninawahakikishia tu kwamba, dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kwamba barabara zinajengwa na zinapitika, na ndiyo maana tumeendelea na taratibu kwamba za kuongeza bajeti katika Halmashauri ya Moshi Vijijini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tutaendelea pia kuhakikisha
kwamba, kwa kadri tunavyopata fedha tunapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ili tuweze kufikia lengo la kuikamilisha kwa kiwango cha lami na changarawe kwa kadri itakavyowezekana.
Name
Moses Ludovico Kaegele
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nkasi Kusini
Primary Question
MHE. EDIBILY K. KINYOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Kata za Asante Nyerere na Kata ya Shunguliba kwa kiwango cha changarawe?
Supplementary Question 7
MHE. MOSES L. KAEGELE: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Nkasi Kusini na hususan Kata ya Kizumbi na Kata ya Ninde, Kijiji cha Lupata, Lyapinda na Msamba havijaunganishwa na aina yoyote ile ya barabara na ni kweli hadi sasa mkandarasi ameshapatikana, lakini hajasaini mkataba.
Je, ni lini Serikali itatoa fedha ili huyu mkandarasi asaini
mkataba na kisha kufungua barabara ya kutoka Lupata – Msamba – Lyapinda ili wananchi waweze kupata usafiri na usafirishaji wa shughuli mbalimbali?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia mara kadhaa kuhusiana na ujenzi na ukarabati wa barabara hizo. Mimi nimhakikishie tu Mheshimiwa mbunge
kwamba, Serikali tunafahamu kwamba tunahitaji kupeleka fedha kwa ajili ya ukarabati wa barabara hizo na tunaendelea na hatua za kibajeti, tuko kwenye hatua ya kutangaza zabuni, lakini tuko kweye hatua pia za kupata fedha kwa ajili ya matengenezo ya dharura.
Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutahakikisha tunazipa kipaumbele barabara hizo ili ziweze kutengenezwa na ziweze kupitika vizuri zaidi. (Makofi)
Name
Pascal Lucas Lutandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chato Kusini
Primary Question
MHE. EDIBILY K. KINYOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Kata za Asante Nyerere na Kata ya Shunguliba kwa kiwango cha changarawe?
Supplementary Question 8
MHE. PASCAL L. LUTANDULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona. Kwa niaba ya wananchi wa Chato Kusini ninaomba kuuliza swali la nyongeza.
Ni lini Serikali itatujengea barabara ya kutoka Iparamasa – Imalamawazo ambayo imekuwa ikisababisha adha kubwa kwa wananchi wa Iparamasa mpaka Imalamawazo na kusababisha ajali kwa siku nyingi? Nini kauli ya Serikali itatujengea hiyo barabara? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Mheshimiwa Lutandula, Mbunge wa Jimbo la Chato Kusini kwa ufuatiliaji wake. Lakini ninafahamu kwamba Halmashauri ya Chato ni moja ya halmashauri ambazo
ziko kwenye mpango wa TACTIC, lakini ninafahamu kwamba tuna hatua nzuri za kwenda kutekeleza Miradi ya TACTIC katika jimbo hilo, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tunafahamu pia bajeti ya TARURA kila mwaka imeendelea kuongezeka kwa ajili ya kufanya matengenezo lakini pia kufungua barabara katika Jimbo la Chato Kusini na Chato Kaskazini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tutaendelea Mheshimiwa Mbunge kuhakikisha kwamba barabara hizo tunazipa kipaumbele zinatengenezwa na kuhakikisha kwamba zinapitika msimu wote wa mwaka na hususan kuanza kuzijenga kwa kiwango cha
changarawe. (Makofi)