Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 47 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 556 2026-06-10

Name

Revocatus Chipando Clayton

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Mjini

Primary Question

MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. CLAYTON R. CHIPANDO auliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga shule tatu mpya za sekondari Jimbo la Kigoma Mjini ikiwemo ya sayansi, sanaa na michezo na shule ya wasichana?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA
SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la mheshimiwa Clayton Revocatus Chipando, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikijenga shule mpya za sekondari nchini na kuongeza miundombinu katika shule zilizopo ili kuendana na ongezeko la wanafunzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2021/2022 – 2025/2026, Serikali imetoa shilingi billioni 5.6 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya nne za sekondari za Businde Mpya, Mjimwema Hill, Kimpampa na Burega, madarasa 152, maabara 24 na kiwanja kimoja cha michezo mbalimbali katika Shule ya Sekondari Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, mpango wa Serikali wa ujenzi wa shule za wasichana ilikuwa shule moja kwa kila mkoa ambapo shilingi bilioni 4.35 zilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Wasichana Kigoma ambayo ilijengwa katika Halmashauri ya Uvinza, Mkoani wa Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2026/2027, Serikali imetenga shilingi milioni 240 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 10 katika shule tano za sekondari Kigoma Ujiji, Rusimbi, Burega, Bushabani na Businde za Jimbo la Kigoma Mjini. Serikali itaendelea kujenga shule mpya na kuongeza miundombinu katika shule za sekondari nchini ikiwemo katika Jimbo la Kigoma
Mjini. Ahsante.