Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ester Amos Bulaya
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. CLAYTON R. CHIPANDO auliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga shule tatu mpya za sekondari Jimbo la Kigoma Mjini ikiwemo ya sayansi, sanaa na michezo na shule ya wasichana?
Supplementary Question 1
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninakushukuru, nami niulize maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Halmashauri ya Mji wa
Bunda tuna shule za kimkakati; Shule ya Dkt. Nchimbi, Shule ya Sekondari Sizaki, Sule ya Sekondari Kabasa, pamoja na Bunda Day zinachangamoto ya mabwalo, maktaba na mabweni. Zinahitajika zaidi ya shilingi bilioni 1.7 ili kukamilisha mahitaji hayo niliyoyataja kwa ajili ya kuongeza ufaulu kwa watahiniwa, ni lini sasa mtatupatia ili tuweze kukamilisha changamoto hiyo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Serikali imekuwa
ikijenga shule za kimkakati za wanawake, za wasichana katika kila mkoa, lakini shule hizi hazina uzio kwa ajili ya kuwalinda mabinti wetu katika shule hizi. Sasa ni lini Serikali, mna mkakati gani wa kuhakikisha hizi shule zote za wasichana za kimkoa zinakuwa na uzio? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimpongeze sana Mheshimiwa Ester Bulaya Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, lakini kwanza ninamthibitishia kwamba, moja ya mpango wa Serikali ni kuhakikisha shule zetu zinakuwa na mabwalo na zile shule za boarding zinakuwa na mabweni lakini na maktaba, kwa sababu miundombinu hii ni muhimu sana katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimhakikishie Mheshimiwa
Mbunge kwamba shule zote alizozitaja tutahakikisha tunaziwekea mpango mkakati wa utekelezaji, lakini hususan shule ambayo inachukua jina la Mheshimiwa Makamu wa Rais, Mheshimiwa Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, tutaipa kipaumbele cha kwanza cha haraka iwezekanavyo kwa hadhi ya kiongozi wetu ili shule hiyo iweze kupelekewa miundombinu hiyo na nyingine tutaendelea kuzitengea bajeti kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. (Makofi)
MWENYEKITI: Mheshimiwa Eric James Shigongo, swali la
nyongeza.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili kuhusiana na uzio kwenye shule za kidato cha tano na sita za mikoa za wasichana, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge shule zile 26 zilizojengwa katika mikoa yetu yote 26, kwanza tulianza ujenzi kwa awamu, tulikamilisha majengo yote muhimu kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 4.4 kwa shule zote, lakini sasa tutakwenda awamu ya pili kwa ajili ya kuanza ujenzi wa fence ili kuweza kuboresha usalama wa wanafunzi katika shule hizo. (Makofi)
Name
Eric James Shigongo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Buchosa
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. CLAYTON R. CHIPANDO auliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga shule tatu mpya za sekondari Jimbo la Kigoma Mjini ikiwemo ya sayansi, sanaa na michezo na shule ya wasichana?
Supplementary Question 2
MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninashukuru kwa kuniona.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Kijiji cha Busikimbi
watoto wao wanatembea kilometa 10 kwenda shule na kilometa 10 kurudi nyumbani. Ulikuwepo mpango wa Serikali kwa kujenga shule ya sekondari katika kijiji hicho katika Kisiwa cha Maisome. Ningependa kufahamu, je, Serikali itajenga lini sekondari hiyo?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimpongeze sana Mheshimiwa Eric Shigongo, Mbunge wa Jimbo la Buchosa, amefuatilia mara kadhaa kuhusiana na shule za msingi lakini pia hata shule za sekondari. Dhamira na mipango ya Serikali ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma umbali mfupi iwezekanavyo ili kuepuka wanafunzi kutembea umbali mrefu na wengine kupata changamoto wakati wa kwenda na kurudi shule.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwa upande wa shule za msingi tunao
mpango wa Mradi wa BOOST ambao tunaendelea kuainisha
maeneo ambayo yana uhitaji wa ujenzi wa shule za msingi na
tutahakikisha tunakupa kipaumbele, lakini kwa mpango wa shule za sekondari, tunao mpango wa SEQUIP, lakini tunao mpango ambao unakwenda kutekelezwa kwa ajili ya kuchukua wanafunzi wa double cohort Januari, 2028.
Kwa hiyo, maeneo yote ambayo yana umbali mkubwa wa
wanafunzi tutahakikisha tunayatambua na tayari
tumekwishayatambua na tutapeleka fedha kwa ajili ya kujenga shule maeneo hayo ili kupunguza umbali wa wanafunzi katika shule zao. (Makofi)
Name
Cornel Lucas Magembe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chato Kaskazini
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. CLAYTON R. CHIPANDO auliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga shule tatu mpya za sekondari Jimbo la Kigoma Mjini ikiwemo ya sayansi, sanaa na michezo na shule ya wasichana?
Supplementary Question 3
MHE. CORNEL L. MAGEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la
nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Halmashauri ya Chato kwa
maana ya Jimbo la Chato Kaskazini, ipo shule ya kidato cha sita ya wasichana inaitwa Ilemela Sekondari ambayo shule ile
imeanza leo takribani miaka mitano, lakini shule ile iko zaidi ya
kilometa 15 kutoka pale kwenda Chato Mjini. Shule ile haina uzio, lakini vilevile haina hata gari la kuweza kuwasaidia watoto wale wanapopata changamoto za kuugua, kuwapeleka hospitali inapotokea.
Je, Serikali ina mpango gani wa kutuwekea uzio katika shule
ile na kutuletea gari kwa ajili ya kuwasaidia watoto wale? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwa bahati nzuri tumekwishaongea mara kadhaa na Mheshimiwa Magembe, Mbunge wa Jimbo la Chato Kaskazini na tulikubaliana kwamba yako maeneo ambayo tuna shule za wasichana, shule mchanganyiko, lakini pia hata shule za wavulana ambao tunahitaji kujenga uzio ili kuboresha usalama wa wanafunzi katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatumia nafasi hii kuwakumbusha
na kuwasisitiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini kwamba waendelee kutenga fedha kwa awamu kupitia mapato ya ndani ya halmashauri kuanza kujenga uzio au fence katika shule zetu ili kuboresha usalama wakati Serikali Kuu inaendelea na mipango kwa ajili ya kuwaunga mkono kuhakikisha kwamba shule zetu zinakuwa na usalama zaidi.
Name
Suma Ikenda Fyandomo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. CLAYTON R. CHIPANDO auliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga shule tatu mpya za sekondari Jimbo la Kigoma Mjini ikiwemo ya sayansi, sanaa na michezo na shule ya wasichana?
Supplementary Question 4
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Shule ya Sekondari Nkunga iliyopo
Wilaya ya Rungwe ina wanafunzi 850, ina bweni moja ambalo
linabeba wanafunzi 80 tu. Wanafunzi walio wengi wanatembea umbali mrefu. Sasa kwa bweni lile la wanafunzi 80 tumeweka watoto wa kike, watoto wa kiume hawana bweni kabisa.
Sasa je, ni lini Serikali itajenga mabweni kwenye shule hiyo ya
sekondari ya Nkunga?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza Mheshimiwa Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalumu, lakini nimhakikishie tu kwamba, kwanza Serikali tumeweka sera na miongozo kwamba shule za kidato cha kwanza hadi cha nne ambazo siyo maalumu kwa maana ya kwamba si shule za bweni, basi hatuweki kipaumbele cha hali ya juu cha kujenga mabweni, isipokuwa kama ni mahitaji hatarishi kama maeneo ya wafugaji na maeneo ya aina hiyo.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nikuhakikishie tu kwamba
kama shule hiyo ina kidato cha tano na sita tutaipa kipaumbele kwa ajili ya kutafuta fedha kwenda kujenga mabweni katika shule hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ikiwa ni shule ya kidato cha kwanza
na cha nne, ikiwa halmashauri wanaona umuhimu wa kuwa na mabweni, ninatumia nafasi hii kumsisitiza Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Rungwe waweke utaratibu wa ndani wa
halmashauri kujenga mabweni katika shule hizo ili wanafunzi
waweze kupata maeneo mazuri zaidi ya kusoma. (Makofi)
Name
Emanuel Qambaji Nuwas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. CLAYTON R. CHIPANDO auliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga shule tatu mpya za sekondari Jimbo la Kigoma Mjini ikiwemo ya sayansi, sanaa na michezo na shule ya wasichana?
Supplementary Question 5
MHE. DKT. EMANUEL Q. NUWAS: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninashukuru kupata nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Halmashauri ya Wilaya ya
Mbulu wananchi wamejenga shule nne za sekondari kutokana na watoto wao kutoka umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 12. Tuna Shule ya Mangisa, Dotina, Aloda na Getanyamba.
Je, Serikali ina mpango gani wa kusaidia kumalizia maboma
na haya madarasa mawili ili shule hizi ziweze kusajiliwa na kusaidia wanafunzi hawa? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa Serikali kwenye uboreshaji wa sekta ya elimu msingi na sekondari ni kuhakikisha kwamba tunakuwa na madarasa ya kutosha kwa ajili ya wanafunzi wetu. Ninaomba nikupongeze Mheshimiwa Dkt. Nuwas, Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, lakini ninawapongeza sana wananchi wa Mbulu Vijijini kwa kuchanga michango yao na kujenga shule hizo nne na
kuanza kudahili wanafunzi kwa ajili ya masomo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimhakikishie tu Mheshimiwa
Mbunge kwamba, kupitia fedha za Serikali za mapato ya ndani ya halmashauri, lakini na Serikali Kuu tunayo mipango ya kuhakikisha maboma yote ambayo yamejengwa katika shule zetu yanakamilishwa na kutumika na tutahakikisha katika utekelezaji wa mpango huo tunazipa kipaumbele shule hizo katika Jimbo la Mbulu Vijijini.
Name
Subira Khamis Mgalu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. CLAYTON R. CHIPANDO auliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga shule tatu mpya za sekondari Jimbo la Kigoma Mjini ikiwemo ya sayansi, sanaa na michezo na shule ya wasichana?
Supplementary Question 6
MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante,
kwanza kwa kuongoza vikao vizuri, lakini kwa kunipa fursa ya ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Kisutu, Jimbo la Bagamoyo
tuna shule moja ya msingi ambayo ilijengwa mwaka 1890, lakini baada ya hatua ya Mheshimiwa Rais kufuta hati ya shamba ya Mchina na kupata ardhi ya kujenga shule, Jumapili iliyopita niliungana na wananchi hao kuanza kujenga shule nyingine ya msingi baada ya ile ya awali kuwa na wanafunzi zaidi ya 1,140 na tulishakamilisha msingi.
Je, Serikali inatupa matumaini gani ya kutuunga mkono
kupitia Mradi wa BOOST ili kuweza kukamilisha shule hii ya msingi? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo na amefuatilia mara kadhaa kuhusiana na mahitaji ya ujenzi wa shule mpya ya msingi katika eneo hilo. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba hiyo ndiyo dhamira ya Serikali na ndiyo mipango ya Serikali. Ninawapongeza wananchi wa Jimbo
la Bagamoyo lakini pia na menejimenti ya Halmasahuri ya
Bagamoyo kwa kuandaa eneo kwa ajili ya ujenzi wa shule
nyingine. Ninatoa wito kwamba Mkurugenzi kupitia mapato ya ndani waanze hatua za awali za ujenzi wa madarasa katika shule hiyo mpya na sisi kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, tutaona namna katika bajeti zetu kwenda kuunga mkono kuhakikisha kwamba shule hiyo inajengwa.
Name
Florent Laurent Kyombo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nkenge
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. CLAYTON R. CHIPANDO auliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga shule tatu mpya za sekondari Jimbo la Kigoma Mjini ikiwemo ya sayansi, sanaa na michezo na shule ya wasichana?
Supplementary Question 7
MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninakushukuru kwa nafasi. Kwanza, niishukuru Serikali kwa ujenzi wa shule za sekondari ndani ya Jimbo la Missenyi, lakini bado uhitaji ni mkubwa katika Kata za Kyaka na Mutukula.
Je, ni lini sasa Serikali itajenga shule za sekondari katika kata
hizo?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango na sera yetu ni kwamba kila kata iwe na shule ya sekondari, lakini kwa zile kata ambazo shule za sekondari zipo, lakini zimekuwa na wanafunzi wengi kupita kiasi, tumekuwa na utaratibu wa kujenga shule nyingine za sekondari ili kuweza kupunguza msongamano katika shule zilizopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Florent Kyombo, Mbunge wa Jimbo la Missenyi
kwamba tutazipa kipaumbele Kata ya Mutukula na Kata ya
Kyaka katika mipango yetu ya ujenzi wa shule za sekondari ili
tuhakikishe huduma ya elimu hiyo inawafikia wanafunzi katika
kata hizo.
Name
Azza Hilal Hamad
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. CLAYTON R. CHIPANDO auliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga shule tatu mpya za sekondari Jimbo la Kigoma Mjini ikiwemo ya sayansi, sanaa na michezo na shule ya wasichana?
Supplementary Question 8
MHE. AZZA H. HAMAD: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Kijiji cha Numbili
kilichopo Jimbo la Itwangi wameanzisha ujenzi wa shule ya
sekondari kwa kujenga vyumba sita vya madarasa na maboma yameshakwishakamilika.
Je, ni lini Serikali italeta fedha kwa ajili ya kukamilisha
majengo haya ili kuwaondolea wanafunzi hawa umbali mrefu
wanaotembea kwenda kutafuta elimu ya sekondari? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, niwapongeze sana wananchi wa Jimbo la Itwangi, na Mheshimiwa Mbunge kwa kuchangia nguvu zao na kujenga madarasa sita kwa ajili ya shule hiyo ya sekondari. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali kupitia mapato ya ndani ya halmashauri na nitumie nafasi hii nimsisitize Mkurugenzi, watenge mapato ya ndani ya halmashauri kwenda kuunga mkono juhudi za wananchi katika ukamilishaji wa miundombinu ya shule hiyo, lakini na sisi Serikali Kuu kupitia Ofisi ya Waziri, TAMISEMI tutaona namna nzuri ya kuhakikisha kwamba shule hiyo
inakamilika mapema iwezekanavyo na kuanza kutoa huduma
kwa wanafunzi kwa kadri ilivyotarajiwa.
Name
Abubakar Damian Asenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilombero
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. CLAYTON R. CHIPANDO auliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga shule tatu mpya za sekondari Jimbo la Kigoma Mjini ikiwemo ya sayansi, sanaa na michezo na shule ya wasichana?
Supplementary Question 9
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninakushukuru sana. Kwa kuwa Halmashauri ya Mji wa Ifakara hatujapata mgao wa shule hadi sasa na kwa kuwa Halmashauri ya Mji wa Ifakara ni halmashauri ya pili kwa ukuajia wa uchumi na ongezeko la watu baada ya Manispaa ya Morogoro, na pia kwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri yangu ameshaandika barua kuomba kusaidiwa kujengewa shule nne kutokana na uhitaji mkubwa wa madarasa; madarasa 20 Kata ya Mwaya, madarasa 18 Kata ya Kibaoni, madarasa 15 Kata ya Ifakara na madarasa 11 Kata ya Viwanja 60.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni nini mpango wa Serikali
kutusaidia ujenzi wa shule mpya hizo katika uhitaji mkubwa huo wa madarasa?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Asenga, Mbunge wa Jimbo la Ifakara kwa kazi nzuri kubwa anayoifanya na ninakumbuka jana tu walikuja hapa mezanitukaongea kuhusiana na uhitaji wa shule hizo na mimi nimemuhakikishia kwamba fedha zilizopelekwa kwenye baadhi ya halmashauri kwa ajili ya shule awamu hii ni awamu ya kwanza, lakini zoezi hili ni endelevu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tutaendelea kupeleka fedha kwa
ajili ya kujenga shule, madarasa na miundombinu mingine katika maeneo yote yenye uhitaji, ikiwemo katika Jimbo la Ifakara.
Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba
madarasa uliyoyataja hayo katika shule hizo tutatoa kipaumbele kuhakikisha kwamba tunapeleka fedha na kujenga na kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wetu.
Name
Hawa Subira Mwaifunga
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. CLAYTON R. CHIPANDO auliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga shule tatu mpya za sekondari Jimbo la Kigoma Mjini ikiwemo ya sayansi, sanaa na michezo na shule ya wasichana?
Supplementary Question 10
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninashukuru kwa kuniona. Shule ya Sekondari Itonjanda,
imeongezwa madarasa matano pamoja na matundu nane ya
vyoo ili kuipanua kuwa high school (kidato cha kwanza mpaka kidato cha sita), lakini mpaka sasa shule hii haijasajili wanafunzi wala haijaanza kufanya kazi kwa sababu hakuna hostel.
Je, nini kauli ya Serikali juu ya kutokufungua shule hii kwa
sababu haina hostel, mtuletee hostel ili watoto wetu wa Kata ya Itonjanda waweze kupata elimu karibu na maeneo yao? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Mheshimiwa Hawa Mwaifunga, Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, lakini nikuhakikishie tu kwamba safari ni hatua, tumeanza na hatua ya kwanza; kwanza dhamira ya
kuipandisha hadhi shule hiyo kuwa kidato cha tano na sita, lakini tumekwenda hatua ya pili ya kujenga madarasa hayo matano na nikuhakikishie kwamba, hatua ya tatu ya kujenga hostel na miundombinu mingine ipo kwenye mipango ya Serikali na tutahakikisha tunaikamilisha ili tuweze kudahili wanafunzi wa kidato cha tano na sita kwa ajili ya manufaa ya elimu katika shule hiyo na jimbo hilo.
Name
Zainab Rashid Kawawa
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. CLAYTON R. CHIPANDO auliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga shule tatu mpya za sekondari Jimbo la Kigoma Mjini ikiwemo ya sayansi, sanaa na michezo na shule ya wasichana?
Supplementary Question 11
MHE. ZAINAB R. KAWAWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninakushukuru kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Shule ya Sekondari ya Anna
Magowa iliyopo Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi, ni shule ya watoto wa kike, lakini haina ukuta, ni shule ya bweni na ina watoto wa kike. Je, ni lini Serikali, itajenga ukuta kwa ajili ya kusaidia watoto wale wa kike wasome kwa usalama?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli katika shule zetu tunahitaji kuboresha sana usalama na hususani kwa kujenga uzio ili wanafunzi wetu wawe katika mazingira bora na salama zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimhakikishie Mheshimiwa
Zainab Kawawa, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Lindi
kwamba hivyo ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali na
tutahakikisha kwenye bajeti zetu za mapato ya ndani ya
halmashauri, lakini fedha Serikali kuu tunazipa kipaumbele shule kama hiyo ili tuhakikishe tunajenga fence na kuboresha usalama kwa wanafunzi wetu.
Name
Agnesta Lambert Kaiza
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. CLAYTON R. CHIPANDO auliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga shule tatu mpya za sekondari Jimbo la Kigoma Mjini ikiwemo ya sayansi, sanaa na michezo na shule ya wasichana?
Supplementary Question 12
MHE. AGNESTA L. KAIZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninakushukuru kwa kuniona.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Shule ya Msingi Darajani iliyopo
Kimanga, ni shule ambayo haina uzio kabisa, lakini ipo
sambamba kabisa na makaburi, kitendo kinachopelekea watoto wetu kushiriki makaburi kuliko jinsi wanavyoshiriki masomo.
Swali langu, ningeomba kufahamu nini mkakati wa Serikali
wa dharura wa kujenga uzio kwenye hii shule ili watoto wetu
waache kushiriki mazishi na badala yake wajikite katika suala zima la kupata masomo? Ahsante sana.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimhakikishie Mheshimiwa Agnesta Lambert, Mbunge wa Jimbo la Segerea kwamba tunatambua changamoto hiyo na kulingana na location ya shule lazima tuweke kipaumbele kujenga fence ili tuwape utulivu wanafunzi katika masomo.
Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie kwamba Ofisi ya Waziri
Mkuu, TAMISEMI, tumelipokea hilo na tutawasiliana na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, tuone uwezekano wa bajeti za ndani za dharura ili angalau tuanze hatua za ujenzi wakati Serikali Kuu inajipanga kwa ajili ya kuunga mkono. (Makofi)