Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 47 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 557 2026-06-10

Name

Shaffin Ahmedali Sumar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uyui

Primary Question

MHE. SHAFFIN A. SUMAR aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara kutoka Malumba- Mabama Centre- Mwigelezi kwa kiwango cha lami?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA
SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Shaffin Ahmedali Sumar, Mbunge wa Jimbo la Uyui kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi na ukarabati wa barabara ili kuboresha usafiri na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi nchini ikiwemo barabara za halmashauri ya wilaya ya Uyui.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ina mpango wa kuijenga Barabara ya Malumba – Mabama Center – Mwegelezi yenye urefu wa kilometa 5.37 kwa kiwango cha lami. Katika mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya kufanya usanifu wa barabara hiyo ili kubaini gharama halisi za ujenzi wa barabara hiyo. Aidha, ujenzi wa barabara hiyo unatarajiwa kufanyika katika mwaka wa fedha 2027/2028.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kujenga na kukarabati barabara zote nchini ili kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo barabara za Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.