Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 47 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 558 | 2026-06-10 |
Name
Abdallah Jafari Chaurembo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbagala
Primary Question
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Masista hadi Rufu Nyampombo ili kuondoa kero kwa wakazi wa Mtaa wa Rufu ambao wanaongezeka kwa kasi?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA
SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah Jafari Chaurembo, Mbunge wa Jimbo la Chamazi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa Barabara ya Masista hadi Rufu Nyampombo yenye urefu wa kilometa 1.6 kwa wakazi wa Mtaa wa Rufu, hususani kutokana na ongezeko la makazi katika eneo hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikiihudumia Barabara ya Masista hadi Rufu kwa kuichonga, kuiwekea changarawe pamoja na kuweka zege katika maeneo korofi. Katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali ilichonga barabara yote, ikaweka changarawe kwa urefu wa meta 820 na kuweka zege meta 168 kwa gharama ya shilingi milioni 104.4. Aidha, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri ya Manispaa ya Temeke iliweka zege kwa urefu wa meta 200 kwa gharama ya shilingi milioni 96.68.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imeweka bajeti ya shilingi milioni 120 kwa ajili ya kuendelea kuboresha barabara hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutafuta rasilimali fedha ili kuiwezesha barabara hii kujengwa yote kwa kiwango cha lami.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved