Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Abdallah Jafari Chaurembo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbagala
Primary Question
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Masista hadi Rufu Nyampombo ili kuondoa kero kwa wakazi wa Mtaa wa Rufu ambao wanaongezeka kwa kasi?
Supplementary Question 1
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa barabara hii imekuwa ikichongwa mara kwa mara na ikifika kipindi cha mvua, barabara hii yote huharibika upya na kupoteza fedha. Je, Serikali haioni ipo haja ya kuijenga barabara hii yote kwa kiwango cha zege ili kuokoa fedha ambazo zimekuwa zikipotea kila mara?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, barabara hii ya Rufu
Nyampombo ni barabara ambayo inaunganishwa na barabara ya Jimbo la Mkuranga. Je, Serikali haioni ipo haja ya barabara hii ya Rufu Nyampombo na zile za Mkuranga zikajengwa ili kuondoa msongamano uliokuwepo Kilwa road?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Abdallah Jafari Chaurembo, Mbunge wa Chamazi na nimhakikishie tu kwamba dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kwamba barabara zetu zote za mijini na vijijini zinapitika msimu wote wa mwaka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatambua kwamba Mheshimiwa
Mbunge, amefuatilia mara kadhaa kuhusiana na ujenzi wa
barabara hii yote kiwango cha lami na tayari Serikali imeanza
kwa awamu tumeshajenga vipande vya changarawe, vipande
vya zege na mpango wa Serikali ni kuhakikisha kwamba
barabara yote inajengwa kiwango cha lami ama zege kulingana na mazingira yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali inaona umuhimu huo na tutatenga bajeti kwa awamu kuhakikisha barabara hii inajengwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili kuhusiana na barabara ya Rufu
Nyampombo ambayo inaunganisha Jimbo la Chamazi na Jimbo la Mkuranga, ni kweli kwamba barabara hii ikijengwa itapunguza sana msongamano wa Kilwa road. Moja ya dhamira ya Serikali ni kupunguza msongamano katika majiji hususani katika Jiji la Dar es Salaam.
Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge
kwamba tumepokea hoja hii, tutaifanyia kazi kwa kuipa
kipaumbele ili angalau tuendelee kupunguza foleni katika
barabara zetu katika Jiji la Dar es Salaam.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved