Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 47 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 559 2026-06-10

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza: -

Je, lini eneo la NDC njia panda ya Machame litaachwa kwa wafanyabiashara ili waweze kulitumia na kuanzisha mji mdogo wa kibiashara?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la NDC lililopo njia panda ya Machame, Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro ni eneo lenye ukubwa wa ekari 229.13 linalomilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC). Serikali imetenga eneo hili maalum kwa ajili ya ujenzi wa kongani ya viwanda ambapo tayari mshauri mwelekezi
ameshapatikana kwa ajili ya zoezi la upangaji wa eneo hilo. Kwa sasa Serikali imewakodishia wananchi eneo hilo kwa ajili ya shughuli za kilimo. Ahsante.