Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 47 Water and Irrigation Wizara ya Maji 561 2026-06-10

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASIA A. HALAMGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga kisima cha maji katika Kata ya Basodesha?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Asia Abdulkarim Halamga, Mbunge wa Jimbo la Hanang, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa Serikali ni kuhakikisha vijiji vyote 1,575 ambavyo havijafikiwa na huduma ya majisafi na salama vinafikiwa na huduma hiyo ifikapo mwaka 2030 ikiwemo Kijiji cha Basodesh kilichopo Kata ya Basodesha Wilaya ya Hanang, Mkoani Manyara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika kijiji hicho, Serikali imekamilisha uchimbaji wa kisima kirefu chenye uwezo wa kuzalisha maji lita 20,000 kwa saa Aidha, usanifu wa miundombinu ya usambazaji maji umekamilika na Serikali inaendelea kutafuta fedha zaidi ya shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kuanza utekelezaji. Mradi huo unatarajiwa kunufaisha zaidi ya wananchi 5,620 wa Kijiji cha Basodesha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, katika hatua za awali za kupunguza changamoto ya maji katika Kijiji cha Basodesha, Serikali katika mwaka wa fedha 2026/2027 itatekeleza mradi wa maji kwa kutumia chanzo cha Ziwa Bassoutu. Mradi huo unatarajiwa kutekelekezwa ndani ya miezi 12 ambapo miongoni mwa maeneo yatakayonufaika ni pamoja na Diling’ang, Endamudayga na baadhi ya sehemu za Vijiji vya Basodesha na Mureru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.