Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASIA A. HALAMGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga kisima cha maji katika Kata ya Basodesha?

Supplementary Question 1

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue nafasi hii
kuipongeza Serikali chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo inaifanya kuendelea kutatua changamoto ya maji katika nchi yetu ya Tanzania.

Swali langu la kwanza, Kata hii ya Basodesha toka dunia imeumbwa hawakuwahi kugusa maji ya bombani, naishukuru Serikali kwa kuchimba visima toka mwaka 2021 lakini hadi sasa usambazaji wa maji haujafanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kazi hii kubwa ya Serikali
iliyofanywa ninaomba kupata commitment ya Serikali sasa kazi hii ambayo imefanyika ni lini wananchi watakunywa maji ya bombani kwa kazi iliyobakia ya usambazaji hasa katika maeneo ya Kijiji cha Basodesha chenyewe, Kijiji cha Gidamo na Kijiji cha
Gisiali ni lini kazi hii itaenda kuanza?

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo langu la pili, je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari kuambatana na mimi na kwenda kuangalia maji wanaokunywa wananchi kwa sasa?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Asia Halamga, Mbunge bingwa kabisa kutoka pale Hanang na nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzuri anayoifanya, lakini pia napenda kusema kwamba suala la usambazaji wa maji kwa aina ya Mbunge Hanang waliye naye na kwa aina ya Mheshimiwa
Rais tuliyenaye Tanzania kazi hiyo haitakuwa ngumu kwenda kuitekeleza kwani ndiyo falsafa ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeshachimba visima vitano katika Jimbo hili la Hanang na katika kata hii ambayo Mheshimiwa Mbunge ameisema ambapo tunafahamu vijiji viwili vinatumia maji kutoka Mlima Hanang, lakini vijiji hivi vitatu ndivyo ambavyo bado usambazaji huujafanyika, lakini nimtoe hofu pamoja na uchimbaji wa visima ambavyo vimeshakamilika Kijiji
hiki cha Basodesha pamoja na hivi vijiji vitatu tayari tumeshafanya usanifu na gharama yake ni shilingi bilioni 4.7 ya kufanya usambazaji mzima wa huduma ya maji safi na salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu Serikali inaendelea kutafuta fedha, tumekuja na mpango wa muda mfupi katika Kijiji cha Basodesha tunaenda kujenga point source ambapo tayari tumeshapata mtu wa kwenda kufanya hiyo kazi na taarifa niliyonayo siku ya tarehe 12 Juni, 2026 tunaenda kusaini mkataba
kwa ajili ya kuanza kujenga hiyo point source. Sasa kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji napenda
nimwelekeze RM ama Meneja wa Mkoa wa Manyara huu mkataba badala ya kusainiwa siku ya tarehe 12 Juni, 2026 ambapo Mheshimiwa Mbunge atakuwa Bungeni usogezwe iwe siku ya wikiendi ambapo Mheshimiwa Mbunge lazima ashiriki katika kusaini mkataba na huu mkataba hautakiwi kusainiwa Mjini
Hanang, unatakiwa upelekwe katika kijiji ambacho mradi unapelekwa ili wananchi wakashuhudie kazi kubwa inayofanywa na Mheshimiwa Mbunge wao chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe maelekezo kwa ma-RM wote nchini, maeneo ambapo miradi mbalimbali inatekelezwa kuweka jiwe la msingi, lakini kuna miradi ambayo ni ya kuzindua kuna kiwango, naelekeza ma-RM wahakikishe kwamba wazinduaji wa miradi wawe ambao wanakuja kutafuta fedha kwa Mheshimiwa
Dkt. Samia Suluhu Hassan ambao ni Waheshimiwa Wabunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Waheshimiwa Wabunge watashiriki katika kuzindua ama kuweka jiwe la msingi kulingana na miradi ambayo tutakuwa tumeipanga badala ya kuita watu wengine ambao hata hawajui pesa inapatikana wapi. (Makofi)

Kwa hiyo, nasisitiza sana hili kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, Waheshimiwa Wabunge ambao wanakuja Bungeni kupambania hizi fedha akiwemo Mheshimiwa Asia Halamga wawe sehemu ya kuhakikisha kwamba wanashuhudia utiaji wa saini, uzinduzi wa miradi na uwekaji wa jiwe la msingi kuhakikisha kwamba ile ownership na wananchi wao washuhudia kwamba kweli mwakilishi wao anafanya kazi yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili mtumishi wa wananchi wa Wana-Hanang amesema mimi ni nani nikatae kuongozana naye kwenda mpaka Hanang, kwenda kuiwakilisha Serikali na kujionea changamoto ya wananchi wa Hanang, niko tayari kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji. Ahsante sana. (Makofi)