Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 47 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 562 2026-06-10

Name

Zuberi Yahya Mfaume

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini

Primary Question

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA K.n.y. MHE. ZUBERI Y. MFAUME aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga upya Kituo cha Polisi Mtamba kilichobomoka mwaka 2014 na shughuli zake kufanyika katika ofisi ya kijiji?

Name

Mohammed Mahmoud Ayoub

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chaani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi napenda kujibu swali la mheshimiwa Zuberi Yahya Mfaume, Mbunge wa Morogoro Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Mtamba, Kata ya Kisemu baada ya kituo cha awali kubomoka kutokana na uchakavu. Ujenzi wa kituo kipya umefikia kwenye hatua ya umaliziaji ambapo kazi iliyobaki ni kuweka vioo vya madirisha na mifumo ya maji safi na maji taka na fedha kiasi cha shilingi 13,000,000 kinahitajika. Fedha hizo zitatolewa na Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro mwezi Julai, 2026.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.