Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Abubakar Damian Asenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilombero
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA K.n.y. MHE. ZUBERI Y. MFAUME aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga upya Kituo cha Polisi Mtamba kilichobomoka mwaka 2014 na shughuli zake kufanyika katika ofisi ya kijiji?
Supplementary Question 1
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana Serikali kwa majibu mazuri na Mheshimiwa Mfaume alikuwa na maswali alikuwa na ombi moja na mimi nitakuwa na maswali mawili madogo ya nyongeza;
Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi la Mheshimiwa Mfaume ni kwamba wakati...
MWENYEKITI: Mheshimiwa Asenga uliza maswali ya nyongeza kama unalo moja uliza moja kama...
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza anasema wakati kituo hicho cha polisi kikiendelea kujengwa, je, Serikali haioni umuhimu wa kupeleka magari ya doria katika tarafa hizo tatu kutokana na uhalifu mwingi kuongezeka kutokana na uchimbaji wa madini na uuzaji wa karafuu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, tunaishukuru Serikali hii ya Watanzania chini ya Chama Cha Mapinduzi kwa ujenzi wa kituo kizuri cha polisi cha Wilaya ya Kilombero tangu Uhuru, kituo cha polisi kimekamilika lakini hakijazinduliwa kwa sababu hakuna
furniture. Je, ni lini Serikali itapeleka pesa kwa ajili ya furniture na kituo hicho kianze kufanya kazi? Ahsante sana.
Name
Mohammed Mahmoud Ayoub
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chaani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na nimpongeze sana Mheshimiwa Asenga kwa niaba ya Mheshimiwa Zuberi kwa maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza lilikuwa ni suala la umuhimu wa kupeleka gari katika kituo hicho au katika kata hizo tatu na hilo ni kutokana na hali ya uhalifu katika eneo hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili kimsingi ni swali namba 563 katika maswali ya leo, lakini kwa sababu limeulizwa kwenye swali namba 562 kama ni sehemu ya swali (b) au swali la nyongeza kwenye swali la msingi napenda kumjibu Mheshimiwa Mbunge kwamba tunaona umuhimu wa kupeleka usafiri kwenye eneo hilo na nimwahidi tu kwamba tutawasiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro ili kuona magari yale yaliyopo katika wilaya kama hayajatosheleza sana, basi tuone namna ya
kuweza kuongeza usafiri kwenye maeneo hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye swali la (b) la uzinduzi wa kituo ambacho tayari kimejengwa lakini kimekosa furniture, nataka nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba tutahakikisha kwamba kwenye mwaka wa fedha 2026/2027 tunapeleka furniture ili kituo hicho kiweze kuzinduliwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha. (Makofi)
Name
Dotto Jasson Bahemu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ngara
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA K.n.y. MHE. ZUBERI Y. MFAUME aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga upya Kituo cha Polisi Mtamba kilichobomoka mwaka 2014 na shughuli zake kufanyika katika ofisi ya kijiji?
Supplementary Question 2
MHE. DOTTO J. BAHEMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kata ya Kabanga Wilaya ya Ngara kuna wananchi walijenga kituo cha polisi kinaitwa Julilwigwa zaidi ya miaka saba kile kituo hakijaanza kufanya kazi na jengo lilishakamilika. Polisi wanasema kwamba kuna baadhi ya kitu ambavyo havikukamilika katika kile kituo kama sehemu ya
kuhifadhia silaha, kuwa na ceiling board ya zege.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa je, Serikali ipo tayari kumalizia kile kituo ili wananchi waendelee kupata usalama katika eneo hilo?
Name
Mohammed Mahmoud Ayoub
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chaani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na nikushukuru na nimpongeze sana Mheshimiwa Dotto kwa kuendelea kufuatilia kwa karibu sana hali ya usalama kwenye jimbo lake hasa katika eneo hili la Kata ya
Ngara. Niwapongeze sana wananchi kwa jitihada walizozichukua za kuhakikisha kwamba wanashirikiana na Serikali kujenga vituo vya polisi ili kuongeza huduma ya usalama kwenye maeneo ya karibu na wao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ombi ambalo amelitoa
Mheshimiwa Mbunge napenda tu kumuahidi kwamba tuko tayari kupeleka watu wetu kufanya tathmini ili kusudi tuweze kujua gharama halisi na hatimaye kuweza kushirikiana na wananchi kumalizia kazi iliyobaki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Name
Esther Nicholas Matiko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Tarime Mjini
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA K.n.y. MHE. ZUBERI Y. MFAUME aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga upya Kituo cha Polisi Mtamba kilichobomoka mwaka 2014 na shughuli zake kufanyika katika ofisi ya kijiji?
Supplementary Question 3
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,
nakushukuru. Ukizingatia Mji wa Tarime unapanuka kwa kasi ambapo maeneo ya pembezoni kama Kata za Kenyamanyori, Kitare, Nyandoto na Nkende yanakuwa na ongezeko kubwa sana la watu, shughuli za biashara, madini na uwekezaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali ina mpango gani wa dharura wa kujenga vituo vya polisi kwenye kata hizi ambazo ni outpost ili kuweza kuimarisha usalama, kuzuia uhalifu, lakini zaidi kusongeza huduma za Jeshi la Polisi hasa Dawati ya Jinsia karibu na wananchi?
Name
Mohammed Mahmoud Ayoub
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chaani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na nimshukuru sana Mheshimiwa Esther Matiko kwa swali lake la msingi na muhimu hasa katika eneo la kata hizi tatu ambazo amezitaja, kwa kweli kuna umuhimu mkubwa wa kuhakikisha kwamba kwenye kata hizo tunajenga
vituo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kwamba kila kata katika nchi hii kwa upande wa Tanzania bara basi tunajenga kituo cha polisi ili kuhakikishia zaidi wananchi usalama wao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kata hizi ambazo amezitaja Mheshimiwa naomba nimwahidi kwamba tutapeleka watu wetu kufanya ukaguzi kuona kati ya kata hizi tatu ni eneo gani kwa dharura tunaweza tukaanza kuweka kituo cha polisi ili kusudi zihudumie na kata za jirani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Name
Shadya Haji Omar
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA K.n.y. MHE. ZUBERI Y. MFAUME aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga upya Kituo cha Polisi Mtamba kilichobomoka mwaka 2014 na shughuli zake kufanyika katika ofisi ya kijiji?
Supplementary Question 4
MHE. SHADYA HAJI OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi hii. Kwa kuwa Serikali inaendeleza jitihada zake za kukarabati vituo vya polisi ambavyo vilipata kadhia, lakini imekuwa inaonekana inachukua muda sana na mitaa imekuwa bila vituo vya polisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali ina mkakati gani wa kumaliza vituo hivi ili ulinzi na usalama uendelee kupatikana katika mitaa yetu?
Name
Mohammed Mahmoud Ayoub
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chaani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na nimshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Shadya Haji Omar kwa anavyofuatilia kwa karibu masuala ya kiulinzi katika maeneo aliyoyataja na hasa kule katika Jimbo la Tumbatu, najua yeye ni mdau kule.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme kwamba jitihada za Serikali za kuhakikisha kwamba tunajenga vituo vya polisi zimewekwa kwenye bajeti yetu ya mwaka 2026/2027 ambapo tumetenga takribani shilingi bilioni 202 kwa lengo la ujenzi, ukarabati wa vituo pamoja na ofisi za Jeshi la Polisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo nataka niwaombe
Waheshimiwa Wabunge; moja, katika randama tuliyowasilisha ya bajeti ya mwaka 2026/2027 tuliainisha kwa kina kila mkoa na eneo gani kwa mwaka wa fedha 2026/2027 tutaweza kujenga vituo
vya polisi. Yale maeneo ambayo yako nje ya randama hiyo, basi yatakuwa yapo kwenye mpango wetu wa miaka mitano wa ujenzi na ukarabati wa ofisi na vituo vya polisi katika kipindi hiki cha miaka mitano.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Name
Muhsin Haji Ussi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Malindi
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA K.n.y. MHE. ZUBERI Y. MFAUME aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga upya Kituo cha Polisi Mtamba kilichobomoka mwaka 2014 na shughuli zake kufanyika katika ofisi ya kijiji?
Supplementary Question 5
MHE. MUHSIN HAJI USSI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Malindi, Wadi ya Mlandege tuna Kituo cha Polisi
cha Makadara ambacho kwa muda mrefu sasa
kimechakaa na kinahitaji kuboreshwa. Kituo hiki cha Polisi Makadara na kinahitaji kuboreshwa, Kituo hiki cha Polisi Makadara kimekuwa muhimili muhimu sana kwa kuwapatia ulinzi wananchi wa maeneo ya makadara na maeneo jirani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Mheshimiwa Waziri ama Mheshimiwa Naibu Waziri atakuwa tayari kuambatana na mimi kukagua miundombinu hiyo ili kwa makusudi Serikali ifanye jitihada ya kufanya ukarabati kituo hicho cha polisi? Ahsante sana.
Name
Mohammed Mahmoud Ayoub
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chaani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Ussi na kwa kweli Kituo cha Polisi anachokiongelea cha Makadara nakijua na kipo mjini na hali yake haiko vizuri sana. Nataka nimwahidi kwamba Serikali iko tayari wakati wowote lakini niombe tu tutoe fursa ya kumaliza Bunge hili na baada ya hapo tupo tayari kuungana na Mheshimiwa Mbunge ili kwenda kutembelea katika Kituo cha Polisi Makadara.
Name
Paschal Inyasi Chinyele
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Dodoma mjini
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA K.n.y. MHE. ZUBERI Y. MFAUME aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga upya Kituo cha Polisi Mtamba kilichobomoka mwaka 2014 na shughuli zake kufanyika katika ofisi ya kijiji?
Supplementary Question 6
MHE. PASCHAL I. CHINYELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Kituo cha Polisi cha Chang'ombe katika Jiji la Dodoma ni moja ya vituo bora kabisa na vya kisasa ambavyo vimejengwa hivi karibuni kwa ushirikiano kati ya Serikali na wananchi. Hata hivyo kituo hiki kinazungukwa na makazi ya watu
waliosongamana.
Je, ni lini Serikali itajenga uzio katika kituo hiki ili kulinda
usalama wa kituo pamoja na mahabusu pamoja na polisi wenyewe?
Name
Mohammed Mahmoud Ayoub
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chaani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na nimshukuru sana Mheshimiwa Chinyele Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye ameulizia kuhusu ujenzi wa uzio wa Kituo cha Polisi cha Chang'ombe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahnsate kwanza nikiri ni kweli Kituo cha Polisi cha Chang'ombe kipo kwenye mzunguko wa makazi na mimi mwenyewe binafsi katika njia zangu zisizo rasmi mara baada ya kuteuliwa tu nafasi hii nikiwa Dodoma nilikitembelea hicho bila
wenyewe hata pia kujua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiri kwamba upo umuhimu kwa mzunguko ule wa wa makazi uliopo kwenye eneo lile na hasa kwa hali halisi ya usalama ilivyo basi kituo hicho kiweze kujengewa uzio. Nataka nimwahidi tu kwamba tuko tayari kuangalia hali ya fedha ya mwaka wa fedha 2026/2027 endapo itaruhusu na kwa sababu pia yeye ni Makamu Mwenyekiti wetu wa Kamati ya NUU kwa hiyo, nimwahidi kwamba tutajitahidi iwezekanavyo tuweze kumsaidia katika eneo hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.