Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 47 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 564 2026-06-10

Name

Kiza Hussein Mayeye

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KIZA H. MAYEYE aliuliza: -

Je, Serikali haioni haja ya kuanzisha Bodi ya Zao la Chikichi na sheria ya zao hili ili kuratibu uzalishaji wake na mnyororo wa thamani?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo inatekeleza Sheria ya Usalama wa Chakula, Sura ya 249 ambayo ilifanyiwa marekebisho kupitia Sheria ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (Cereals and Other Produce Act), Na. 19 ya Mwaka 2009 na hivyo kuanzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) lengo likiwa ni kusimamia na kuratibu shughuli za uzalishaji, uchakataji, uhifadhi, masoko na biashara kwenye tasnia ya mazao ya nafaka na mazao mchanganyiko likiwemo zao la chikichi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu mkubwa wa zao la chikichi katika kukuza uchumi na kuongeza ajira kwa wananchi. Mafuta yanayotokana na zao hili yanachangia takribani 60% ya mafuta ya kula yanayoagizwa kutoka nje ya nchi hali inayoonesha kuwa zao hili lina fursa kubwa ya uzalishaji wa bidhaa mbadala wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje na hivyo kuokoa matumizi ya fedha za kigeni kuagiza kutoka nje ya nchi.