Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kiza Hussein Mayeye

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KIZA H. MAYEYE aliuliza: - Je, Serikali haioni haja ya kuanzisha Bodi ya Zao la Chikichi na sheria ya zao hili ili kuratibu uzalishaji wake na mnyororo wa thamani?

Supplementary Question 1

MHE. KIZA H. MAYEYE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ninaomba kuuliza maswali ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndani ya Mkoa wa Kigoma, Jimbo la Kigoma Kaskazini ndio linaongoza kwa kilimo cha mawese, lakini wakulima hawa wamekuwa wakitumia zana hafifu za uchakatishaji wa kupata mawese.

Je, Serikali ni lini mtaona umuhimu wa kuwasaidia wakulima wa mawese japo kuwapa mashine ili waweze kuzalisha mawese yenye tija? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili kwa historia kilimo cha mchikichi leo Malaysia ni nchi ya pili kwa kuzalisha mafuta duniani, mbegu walitoa katika Jimbo la Kigoma Kaskazini. Serikali mmekuwa mkitumia pesa nyingi sana za kigeni kuagiza mafuta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini Serikali mtaona umuhimu wa kuleta sheria ya zao la mchikichi ili kuwahakikishia wawekezaji wa viwanda katika mafuta ya mawese? Ahsante. (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimpongeze sana dada yangu Kiza Mayeye, Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa maswali ya msingi sana yenye faida kwa wananchi wa jimbo lake, lakini na Wana-Kigoma kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo moja ambalo nimthibitishie, kwamba moja tunatambua umuhimu wa zao la chikichi na ndio maana ukiangalia hata katika bajeti ambayo mlipitisha hapa ya Wizara ya Kilimo mwaka huu katika mazao manne miongoni mwa
zao ambao tumelipa kipaumbele ni zao la chikichi na
tunakwenda kuzalisha karibu miche milioni tatu ambayo itakusudiwa kugaiwa bure kwa wananchi ambayo itasaidia kuongeza tija katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo maelekezo ya Wizara kwa Bodi ni kuhakikisha kwamba wanapeleka mashine hizi ndogo ndogo kwa ajili ya kuchakata mafuta ili waweze kuongeza thamani kwa wananchi. Kwa hiyo, tayari hilo jambo lipo katika
mpango na tutalitekeleza katika mwaka unaokuja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini umuhimu wa zao la chikichi tunafahamu na ninafikiri kama nilivyosema kwamba hatua ya kwanza sasa tunataka tuongeze uzalishaji na hatua ya pili maana yake sasa tutatengeneza sheria ambazo zitasaidia kulifanya zao
lile kuwa bora ikiwemo kutengenezea sheria katika hatua inayofuatia. Ahsante sana.

Name

Asha Salum Motto

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KIZA H. MAYEYE aliuliza: - Je, Serikali haioni haja ya kuanzisha Bodi ya Zao la Chikichi na sheria ya zao hili ili kuratibu uzalishaji wake na mnyororo wa thamani?

Supplementary Question 2

MHE. ASHA S. MOTTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Mikoa ya Kusini kwa maana ya Mtwara na Lindi imekuwa ikifanya vizuri sana kwenye kilimo cha ufuta na mbaazi. Je, ni lini Serikali itaunda bodi kwa ajili ya mazao haya ili kuleta tija na thamani kwa wakulima wa mikoa hii ya Kusini? Ahsante. (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na nimpongeze vilevile dada yangu Mheshimiwa Asha Motto kwa kazi nzuri ya kuwatetea watu wa Mtwara na sisi kama Wizara tunatambua kwamba mazao ya ufuta na mbaazi ni miongoni mwa mazao ambayo yamekuwa yakifanya vizuri sana
katika kipindi cha kama miaka miwili, mitatu iliyopita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kwa sasa mazao haya yanahudumiwa na Bodi ya COPRA lakini tunaendelea kuangalia tija, maana yake tukiona kama zao linaweza kusimama lenyewe basi Serikali inaweza kulifikiria na kulitafutia bodi katika miaka inayokuja mbele, lakini kwa sasa mazao haya yapo chini ya Bodi
ya COPRA. Ahsante.