Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 47 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 565 2026-06-10

Name

Alan Thomas Mvano

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kakonko

Primary Question

MHE. ALAN T. MVANO aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka zana za kilimo katika Wilaya ya Kakonko ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo inaendelea kutekeleza mpango wa uanzishaji wa vituo 1,000 vya kutoa huduma ya zana za kilimo kwa wakulima katika ngazi ya kata ifikapo mwaka 2030. Lengo likiwa ni kusogeza na kuwawezesha wakulima kupata huduma za zana za kilimo kwa wakati na gharama nafuu ili kuongeza uzalishaji na tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza hilo, Wizara imeanzisha vituo 79 katika halmashauri mbalimbali nchini na utekelezaji unaendelea. Aidha, trekta 340 zimenunuliwa na kusambazwa katika vituo hivyo ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za zana za kilimo kwa wakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2026/2027 Wizara inaendelea na ununuzi wa zana za kilimo kwa ajili ya kuimarisha na kuanzisha vituo vya kutoa huduma za zana za kilimo kwenye halmashauri mbalimbali ikiwemo Kankoko ili kusogeza huduma na kuhamasisha matumizi ya zana za kilimo nchini.