Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Alan Thomas Mvano

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kakonko

Primary Question

MHE. ALAN T. MVANO aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka zana za kilimo katika Wilaya ya Kakonko ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo?

Supplementary Question 1

MHE. ALAN T. MVANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza kabisa niishukuru Serikali kwa majibu mazuri yenye matumaini kwa wananchi wa Kakonko kwamba sasa zana za kisasa za kilimo zinakwenda kupelekwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri hayo ninayo mambo mawili; jambo la kwanza; kwa kuwa zaidi ya 80% ya wananchi wa Kakonko ni wakulima na wamekuwa wakitumia jembe la mkono kwa muda mrefu, pamoja na mikakati mikubwa
ambayo tukonayo ikiwa ni pamoja na mradi mkubwa wa zao la parachichi ambapo tumetenga zaidi ya ekari 1000, vilevile pamoja na mazao mengine ya kimkakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni upi sasa mpango wa Serikali wa haraka kuhakikisha kwamba katika msimu huu wa kilimo unaoanza zana hizi za kisasa zinapelekwa ili kazi hii iweze kuanza hasa katika mradi huu wa ekari 1000 lakini pamoja na kuwasaidia
wananchi wengine?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ni kwamba pamoja na miradi hii ya kimkakati nilikuwa ninamuomba Mheshimiwa Waziri kama atakuwa tayari afike sasa Kakonko kipindi hiki kifupi kinachokuja ili kutembelea maeneo haya ya miradi na kuweza
kuzungumza na wananchi kwa ajili ya kuona namna ya kuongeza tija katika mazao yetu. Ahsante. (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimpongeze vilevile kaka yangu Alan Mvano, Mbunge wa Kakonko kwa maswali yake ya msingi kwa ajili ya wananchi wake na nimthibitishie tu kwamba katika mpango wa haraka kwa sababu katika mwaka wa fedha 2026/2027 Wizara tunanunua zana za kilimo, kwa hiyo, baada ya kufika katika ule mgao basi Halmashauri ya Kakonko itakuwa sehemu ya wale ambao tutawapa mgao mwanzoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuhusu kufika katika eneo lake niko tayari mara baada ya Bunge kuahirishwa nilishahidi kufika Mkoa wa Kigoma nitakwenda Jimbo lako Kigoma Mjini, Kigoma Kaskazini na maeneo mengine yote ili kuhakikisha
kwamba tunawafikia wananchi, tunazungumza nao na
kuwahudumia kama ambavyo ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais. Ahsante.