Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 47 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 566 2026-06-10

Name

Dr. Regina Christopher Malima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. REGINA C. MALIMA aliuliza: -

Je, lini Serikali itatunga sheria ya kuwalinda wazawa katika miradi ya uvuvi na vizimba?

Name

Amb. Dr. Bashiru Ally Kakurwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana, ninaomba kujibu swali la namba 566 la Mheshimiwa Dkt. Regina Christopher Malima, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Sheria ya Uvuvi, Sura 279 na Sheria ya Usimamizi na Uendelezaji wa Uvuvi katika Bahari Kuu, Sura 388 inawalinda Watanzania katika utekelezaji wa miradi ya uvuvi na ufugaji wa samaki kwa vizimba ambapo sheria imezuia wageni kufanya baadhi ya shughuli kama vile uvuvi katika maji ya ndani na biashara ya baadhi ya mazao kama vile kaa na kambakochi hai ili zifanywe na Watanzania pekee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeweka unafuu wa gharama za leseni na tozo mbalimbali kama vile vibali vya uvuvi wa bahari kuu, biashara ya mazao ya uvuvi na ufugaji wa samaki kwa vizimba kwa Watanzania ikilinganishwa na kiasi kinachotozwa kwa wageni. Lengo la hatua hizi za kisheria ni kuwalinda Watanzania kwa kuweka unafuu wa gharama na mazingira rafiki ya ushindani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi
itaendelea kufanya maboresho ya sheria kadri inavyohitajika ili kuhakikisha kuwa Watanzania wanaendelea kulindwa katika utekelezaji wa miradi ya uvuvi na ufugaji samaki kwa vizimba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.