Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 47 | Health and Social Welfare | Wizara ya Afya | 567 | 2026-06-10 |
Name
Abdulaziz Mohamed Abood
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Morogoro Mjini
Primary Question
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD aliuliza:-
Je, lini Serikali itaondoa malipo yasiyo rasmi kwa wajawazito ikiwemo gharama za vifaa wanapokwenda kujifungua?
Name
Dr. Florence George Samizi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Muhambwe
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Afya naomba kujibu swali la Mheshimiwa Abdul-Aziz Mohamed Abood, Mbunge wa Morogoro Mjini kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatekeleza Sera ya Afya ya mwaka 2007 inayoelekeza kutoa huduma za matibabu bure kwa makundi maalum ikiwemo akinamama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano pamoja na wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 wasio na uwezo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeshatangaza rasmi kuanza utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote Awamu ya Kwanza itakayohusisha makundi ya wananchi ikiwa ni pamoja na watoto, wajawazito, walemavu na wazee wasio na uwezo ambapo kundi hili litagharamiwa na Serikali. Kukamilika kwa hatua hii itawezesha wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kupata huduma za afya kwa kugharamiwa na Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe rai kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Waganga Wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya kuhakikisha wanatekeleza maelekezo ya Serikali katika kuhakikisha wajawazito wanapata huduma za afya pasipo kikwazo cha fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved