Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Abdulaziz Mohamed Abood
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Morogoro Mjini
Primary Question
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD aliuliza:- Je, lini Serikali itaondoa malipo yasiyo rasmi kwa wajawazito ikiwemo gharama za vifaa wanapokwenda kujifungua?
Supplementary Question 1
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini hali ilivyo katika Manispaa ya Morogoro siyo hivyo. Wajawazito wanapokwenda kujifungua kwenye vituo vya afya, hospitali ya wilaya au hospitali ya mkoa huwa wanatozwa gharama za ziada za gharama
chungumzima ili waweze kutimiziwa haja yao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, kuna wagonjwa wanaokwenda usiku katika vituo vya afya na hospitali za wilaya na mkoa saa sita, saa saba ya usiku hapewi huduma anaambiwa akalipie control number saa saba ya usiku anaipata wapi control number kulipia? Sasa naomba kauli ya Serikali kuhusu maswali
yangu hayo. (Makofi)
Name
Dr. Florence George Samizi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Muhambwe
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Abood Mohamed kwa kazi nzuri anayoifanya Mkoani Morogoro, tumemuona mara
nyingi akichangia vifaa vya kutolea huduma ya afya kwa wananchi wake na akiunga mkono jitihada za Serikali, tunampongeza sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye maswali yake;
kwanza kabisa naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anagharamia gharama za hawa wanawake. Tunatumia zaidi ya shilingi bilioni saba kununua vifaa vya kujifungua hawa wakina mama ikiwemo dawa za kuzuia kutoka damu nyingi, dawa za kuongeza damu,
chanjo na huduma zote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, hospitali zote nchini hazitakiwi kuwa-charge hawa wanawake huduma hizi kwa sababu tayari Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekwishakulipia hizo gharama. Kwa hiyo, naomba nitoe rai kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Morogoro na vituo vya afya vyote Morogoro wafuate Sera ya Afya ambayo inawataka kutoa huduma bure.
Mheshimiwa Mwenyekiti, isitoshe wote tumeshuhudia
Mheshimiwa Waziri Mkuu akitolea maelekezo jambo hili kila wakati kwamba wajawazito wasilipishwe hizo gharama. Kwa hiyo, naomba wasifanyekazi kwa mazoea badala yake watekeleze huduma ya kumuhudumia mama na mtoto kama Sera ya Afya
inavyoelekeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, wagonjwa
wanaokwenda usiku wanaambiwa control number. Huduma za afya ni masaa 24. Hakuna wakati wowote ambapo huduma inafungwa kwa kusema ni usiku au ni mchana, ndiyo maana tunaingia kwa shift.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tena Mganga Mkuu wa Hospitali ya Morogoro ambaye anawaambia wagonjwa control number usiku na huduma hiyo haipo, ahakikishe anaweka mtalaamu wa mfumo usiku huo ili control number iweze kupatikana wakati wote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, control number isiwe kikwazo cha kumfanya mama asipate huduma, kwa sababu Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshaelekeza lazima tuwahudumie hawa akinamama kwa upendo na furaha ili tuhakikishe kwamba tunafikia malengo ya SDGs kupunguza vifo vya mama na mtoto
kama ambavyo inatarajiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Name
Agnes Elias Hokororo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD aliuliza:- Je, lini Serikali itaondoa malipo yasiyo rasmi kwa wajawazito ikiwemo gharama za vifaa wanapokwenda kujifungua?
Supplementary Question 2
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini ukweli ni kwamba katika vituo vingi vya kutolea huduma za afya bado wajawazito na watoto wadogo wanapokwenda kupata matibabu wanatozwa fedha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatamani kusikia kauli ya Serikali kwa nchi nzima ili vitendo hivi visiendelee kujitokeza katika maeneo mengi. (Makofi)
Name
Dr. Florence George Samizi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Muhambwe
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi kwamba Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan analipa shilingi bilioni saba kila mwaka kwa ajili ya akinamama wajawazito na watoto ili wapate huduma hizi bure. Naomba nielekeze kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Afya, nielekeze Waganga Wakuu kama nilivyosema kwenye jibu langu, Waganga Wakuu wote wa Hospitali zote nchi nzima kuanzia ngazi ya Taifa, Kanda, Mkoa, Wilaya, Vituo vya Afya hadi Zahanati ni marufuku kumtoza mama mjamzito na mtoto chini ya miaka mitano gharama za matibabu kwa sababu Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekwishalipa kwa ajili ya kundi hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved