Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 47 Health and Social Welfare Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 568 2026-06-10

Name

Catherine Canute Joachim

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CATHERINE C. JOACHIM aliuliza:

Je, upi mpango wa Serikali wa kuimarisha malezi na ulinzi wa watoto na vijana ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili na mienendo hatarishi?

Name

Dr. Dorothy Onesphoro Gwajima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA
MAKUNDI MAALUM alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, katika kuimarisha malezi na ulinzi wa watoto na vijana ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili na mienendo hatarishi Serikali inafanya yafuatayo:-

(i) Inatekeleza Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ya miaka mitano kuanzia mwaka 2021/2022 ili kila mtoto wa umri chini ya miaka nane apate huduma jumuishi za malezi na makuzi.

(ii) Vilevile inaendelea na utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya kuwekeza katika afya na maendeleo ya vijana balehe wenye umri wa miaka tisa hadi kumi na tisa.

(iii) Vilevile inatekeleza Mpango Kazi wa Pili wa Taifa wa miaka mitano wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kuanzia mwaka 2024/2025.

(iv) Imezindua mkakati wa kitaifa wa miaka 10 wa kukabiliana na mmomonyoko wa maadili kuanzia mwaka 2026/2027; na mwishio

(v) Imeanzisha Kamati ya Kitaifa ya Ushauri juu ya Usalama wa Mtoto Mtandaoni na tayari imeanza kujadili uwezekano wa kuchuja na kuzuia maudhui yasiyofaa kwa watoto wanapotumia mitandao, pia uwezekano
wa kuwa na laini maalum ya simu kwa watoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua hizi zote ni shirikishi kisekta na kijamii na utekelezaji unaanzia ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa hadi Taifa.