Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Catherine Canute Joachim

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CATHERINE C. JOACHIM aliuliza: Je, upi mpango wa Serikali wa kuimarisha malezi na ulinzi wa watoto na vijana ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili na mienendo hatarishi?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. CATHERINE C. JOACHIM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naipongeza Serikali kwa kuweka jitihada mbalimbali ili kuweka ulinzi kwa watoto na vijana. Pamoja na jitihada hizo nina maswali mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa Serikali imezindua mpango wa miaka kumi wa kukabiliana na mmomonyoko wa maadili; je, nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kunawekwa mifumo katika ngazi ya Serikali za Mitaa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili litakwenda katika Kamati ya Ushauri wa Usalama wa Watoto Mitandaoni. Je, upi mkakati wa Serikali wa kuwajengea uwezo wazazi pamoja na walezi ili waweze kujua jinsi gani watawalea watoto wao katika masuala mazima ya teknolojia? Ahsante.

Name

Dr. Dorothy Onesphoro Gwajima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Catherine Canute Joachim.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na swali la nyongeza la kwanza mkakati gani kuhusu utekelezaji wa mpango wa Taifa wa kudhibiti mmomonyoko wa maadili?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati umeanzia kwenye
Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo mkakati huu utakwenda sambamba na kuunda Kamati za Maadili kuanzia kijijini, kata, halmsahauri na mkoa na hadi ngazi ya Taifa. Kote huko Wajumbe wa Kamati hizi watakuwa ni shirikishi wakiwemo viongozi wa dini,
viongozi maarufu wa kijamii, wawakilishi wa wananchi kwenye maeneo husika, sekta binafsi itakuwepo, mashirika yasiyo ya kiserikali na asasi za kiraia kifupi clusters zote za makundi ya kijamii yatakuwa yamewakilishwa pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana hiyo sasa hizo taarifa zitokanazo na Kamati hizi zinakwenda kuunganishwa na Mabaraza ya Maendeleo ya Kata hadi kwenda kwenye Halmashauri kwenye vikao vyake vyote hadi DCC pale kwa Mkuu wa Wilaya ambaye ndiyo atakuwa Mwenyekiti kila Wilaya hadi mkoani. Kwa hiyo, huku Taifa kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu –
TAMISEMI tutakuwa tunapokea majumuisho yote na
mapendekezo yote ili tuweze kufanyakazi moja ya ku-edit au kuboresha ile mipango kitaifa pamoja na sera na sheria zinazohusu eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la ulinzi wa watoto wanapotumia mitandao ya kijamii, wazazi na walezi wameshirikishwa vipi? Tayari tumeshaanza utekelezaji wa mikakati mbalimbali ikiwemo tumetoa mafunzo kwa wawezeshaji (trainer of trainee) zaidi ya mia tano, ambao hawa tayari wameishaanza
kufundisha walimu mashuleni pamoja na wanafunzi na vikundi vingine vya kijamii kuhusu kuhakikisha watoto wanaelezwa juu ya kutumia mitandao kwa usalama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi karibia wanafunzi milioni 1.8 hivi wameshapata hayo mafunzo na programu inaendelea na tunatarajia kwamba hawa trainer of trainees zaidi ya 500 ambao wametokea pia kila wilaya watashusha chini mpaka kwenye kata kadri ya upatikanaji wa rasirimali za kwetu.

Name

Fatma Ally Rembo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CATHERINE C. JOACHIM aliuliza: Je, upi mpango wa Serikali wa kuimarisha malezi na ulinzi wa watoto na vijana ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili na mienendo hatarishi?

Supplementary Question 2

MHE. FATMA A. REMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapomwezesha mtoto wa kike
tusimsahau pia mtoto wa kiume ambaye pia anakutana na changamoto nyingi za malezi. (Makofi)

Je, Serikali ina mpango gani maalum au mkakati gani
maalum wa kuhakikisha kijana wa kiume anajengwa na kulinda ili aweze kuja kuwa kiongozi bora na baba bora wa kesho? (Makofi)

Name

Dr. Dorothy Onesphoro Gwajima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na nampongeza sana Mheshimiwa Fatma kwa swali lake la nyongeza zuri ambalo linapenda kujua ushiriki wa watoto wa kiume kwenye masuala haya ya malezi na makuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kusema kwamba watoto wote ambao wanasimamiwa chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maluum ni wa jinsia zote na katika mikakati yote tunapotamka neno mtoto, mtoto wa kiume anakuwa ni sehemu. Mfano tunatekeleza mkakati wa vikundi vya
malezi vya wazazi, wazazi hawa wanafundishwa jinsi ya kwenda kufanya malezi na makuzi ya watoto, ndani mle wanaume wapo ambao ni baba zao na hawa watoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatekeleza elimu kwa jamii
inayohusu masuala yanasema Familia Bora Taifa Imara. Tayari wazazi ambao wameshiriki kwenye hii programu au hii kampeni ni kama 550,000 na nusu hivi lakini kati yao laki moja hamsini na saba na pointi ni wanaume.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunawafikia watoto hawa kupitia wazazi wao wa kike na kiume, lakini tukienda mashuleni tuna madawati ya ulinzi wa watoto, madawati ya ulinzi wa watoto ni watoto wote wa kike na kiume, na kwenye uongozi pale kiongozi ni mwanamke na mwanaume kwa pamoja. Kuna
mabaraza ya watoto tunayafanya. Haya mabaraza ya watoto yanaanzia kijijini, kwenye mitaa, kwenye kata. Haya nayo ni watoto wote wako mle ndani. Tumekuwa na watoto wa kutosha wa kiume wanakwenda kuwakilisha nje ya nchi wakitokea kwenye haya mabaraza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiiangalia sheria ya mtoto
ilivyojengwa, inamshughulikia mtoto wa kike na wa kiume. Kwa hiyo, ninapenda tu kusema kwa ufupi tunazingatia masuala haya na ili kuongeza nguvu zaidi tumesajili vyama vya wanaume mbalimbali na siku hiyo nilipowasilisha bajeti tarehe 01 Juni walikuwepo. Lengo ni kuuchukua mtandao wa wanaume uingie, ushike nafasi yake katika kuangalia maslahi ya wanaume, siyo
wakubwa tu bali na watoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na hapa Mheshimiwa Baba Levo tunatarajia kumteua awe Balozi wa Wanaume, lengo ni kwamba kupitia uwezo wake wa kuzungumza nao na kushirikiana nao watuletee zile hoja, wapi tuna-miss point katika kusuka mikakati yetu. Hili linakwenda sambamba na Mheshimiwa Kampala pia. Hawa tumewaona wanaweza wakatusaidia sana kwenda vizuri kwenye hii Wizara, ili hili suala mwishowe lipate majibu ya kutosha na ya kina yanayowaridhisha Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Name

Jamila Mahmoud Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CATHERINE C. JOACHIM aliuliza: Je, upi mpango wa Serikali wa kuimarisha malezi na ulinzi wa watoto na vijana ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili na mienendo hatarishi?

Supplementary Question 3

MHE. JAMILA MAHMOUD JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, na mimi nichukue fursa hii kuipongeza Wizara ya Jinsia kwa kazi kubwa ambayo inaifanya na ninapenda kuchangia kwamba, tunajua kwamba

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kuuliza swali langu, ninajua kwamba Serikali imekuwa ikifanya kazi kwa karibu sana na asasi za kiraia hasa zile ambazo zinajishughulisha na masuala ya ulinzi wa mtoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu linaelekea, je, Serikali ina mikakati gani sasa ya kushirikiana moja kwa moja na zile asasi au NGOs ambazo zinafanya kazi katika masuala ya ulinzi wa mtoto, lakini pia masuala ya elimu na ukuaji wa mtoto? Ninajua kwamba ziko hizi asasi ambazo zinajikita moja kwa moja na haya masuala. Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Dorothy Onesphoro Gwajima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kunipa fursa ya kujibu swali zuri la Mheshimiwa Jamila analotaka kufahamu ushirikiano wetu kati ya asasi za kiraia kwenye masuala
ya ulinzi wa mtoto pamoja na elimu kwa ujumla wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kusema kwamba
ushirikiano unaanza kwa mujibu wa Sheria ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na uendeshaji wake ambapo ngazi ya kitaifa tunalo Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambalo lilipoingia kwenye kipindi hiki cha utekelezaji wa Serikali ya Awamu ya Sita
tuliwataka waupitie upya mwongozo wao wa shirikiano ya hili baraza lote na Serikali. Wameuhuisha na mara baada ya Bunge hili tutauzindua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ni kwamba Kamati za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuanzia ngazi kule yanakotekeleza zinakuwa sehemu ya vikao vyote vya Serikali kuanzia ngazi ya kata, wanaingia pale kama wawakilishi wa NaCoNGO, wanaleta mipango na mikakato yao na taarifa zao zote na kwenye ngazi
ya halmashauri, Mkuu wa Wilaya ndiyo mwenyekiti,
anamwakilisha Mheshimiwa Rais eneo hilo. Kwenye ngazi ya mkoa ni Mkuu wa Mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwenye RCC, kwenye DCC, kwenye Ward DC kule kwenye kata, hawa watakuwa wanakwenda baada ya kuzindua huu mwongozo mapema Julai hii.

Kwa hiyo, hata Kitaifa tumekuwa na vikao nao
tunawaambia msije kwenye vikao vyetu kabla ninyi wenyewe hamjakaa kama NaCoNGO ngazi zote mkaongea yale mnayotaka kuwasilisha Serikalini chini ya Afisa Maendeleo ya Jamii kama mwakilishi wetu huko kwenye ngazi zenu ili mkija Serikalini mje na hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kuanzia kipindi kijacho cha Kamati za Bunge letu tutaanza kuwasilisha taarifa ya utekelezaji. Wamesema nini kutoka ngazi zote, kipi tufanye Kitaifa na kipi wamekwama huko. Ahsante.

Name

Thomas Maganga Kampala

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Primary Question

MHE. DKT. CATHERINE C. JOACHIM aliuliza: Je, upi mpango wa Serikali wa kuimarisha malezi na ulinzi wa watoto na vijana ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili na mienendo hatarishi?

Supplementary Question 4

MHE. THOMAS K. MAGANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwanza ninamshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kuniteua, na mimi ninamshukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tamasha linaandaliwa sasa hivi Dar es Salaam na muandaaji wa tamasha hilo mienendo yake mitandaoni imekuwa haiendani na maadili ya Mtanzania. Serikali imefuatilia kujua maudhui ya tamasha hilo, kwa sababu ikipelekea hivi tunavyoongea ukitazama mitandaoni muandaaji
wa tamasha hilo kwenye picha zake za mjongeo za mtandaoni ameweka mpaka matiti wakati anaandaa tamasha hilo? Nini kauli ya Serikali kwa mwandaaji wa tamasha hilo? (Makofi)

Name

Dr. Dorothy Onesphoro Gwajima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kunipa fursa kujibu swali zuri la Mheshimiwa Kampala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda nikiri kusema kwamba
uratibu wa matamasha mbalimbali una milango mingi ya kuingia na kufanyika. Sasa ninapenda kupata taarifa zaidi pengine huenda ni tamasha liko chini ya sekta ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo au ni la sekta ipi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, approval ya matamasha yote
huwa inafuata miongozo ya kisekta ambako ajenda husika inakwenda kufanyika kwenye hiyo sekta. Ninamwahidi mimi ninafuatilia taarifa kutoka kwake nijue, halafu nitawasiliana na sekta husika kama hilo lipo na kwamba tamasha hilo ni tishio kwa maadili yetu humu Tanzania, kifuatacho itabidi walioli-approve
wawajibike kwa mujibu wa sheria. (Makofi)