Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 44 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 518 2026-06-05

Name

Kassim Hassan Haji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanakwerekwe

Primary Question

MHE. KASSIM HASSAN HAJI aliuliza: -

Je, lini Serikali italeta narekebisho ya sheria ili kuondoa changamoto zinazoendelea katika utekelezaji wa Mfuko wa Jimbo?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Kassim Hassan Haji, Mbunge wa Jimbo la Mwanakwerekwe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo ulianzishwa kwa nia ya kuchochea shughuli za maendeleo katika jimbo. Madhumuni ya mfuko huu ni kuwawezesha Wabunge, kupitia Kamati za Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo kuchangia shughuli za miradi ya maendeleo inayobuniwa na wananchi katika Mpango wa Fursa na Vikwazo (O&OD) na kuidhinishwa na halmashauri.

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza azma hii, mwaka 2009 Bunge lako lilitunga Sheria ya Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo (The Constituencies Development Catalyst Fund Act) Sura ya 96 ambayo imeanzisha Mfuko pamoja na Kamati ya Kuchochea Maendeleo ya Jimbo ili kuweza kutekeleza kwa ufanisi sheria hiyo. Tarehe 5 Februari, 2010 kanuni ya kuweka utaratibu wa kusimamia na kuratibu miradi ya maendeleo itakayoanzishwa katika majimbo ziliandaliwa.

Mheshimiwa Spika, kufuatia hoja ya marekebisho ya sheria Serikali iko tayari kuanisha maeneo au vifungu vya sheria ambavyo vinachangamoto katika utekelezaji wa Sheria ya Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo ili viweze kufanyiwa kazi pamoja na maoni mengine yatakayotolewa na wadau kuhusu sheria hiyo.

Mheshimiwa Spika, ninaomba kuwasilisha.