Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kassim Hassan Haji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanakwerekwe

Primary Question

MHE. KASSIM HASSAN HAJI aliuliza: - Je, lini Serikali italeta narekebisho ya sheria ili kuondoa changamoto zinazoendelea katika utekelezaji wa Mfuko wa Jimbo?

Supplementary Question 1

MHE. KASSIM HASSAN HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana na ninamshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake, lakini ninaomba nimuulize.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa sheria hizi za manunuzi za Mfuko wa Jimbo wa Tanzania bara na Zanzibar zinakinzana na kwa kuwa Wabunge wengi wa Zanzibar wanaingiziwa pesa hizo katika halmashauri; je, ni lini sasa Serikali itakuja na muswada huo hapa ili kurebisha kuondoa shida ambayo ipo kwa muda mrefu? Ahsante sana.

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge Kassim kama alivyoliuliza na nimpongeze kwa kuleta hoja hii na swali hili.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI tumeendelea kupokea maoni ya wadau mbalimbali, Kamati za Bunge, lakini pamoja na baadhi ya Wabunge ambao wametuletea maoni Ofisi wa Waziri Mkuu, TAMISEMI kuhusiana na sheria hii na namna ya kuratibu mfuko huu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishe Mheshimiwa Kassim pamoja na Wabunge wengine kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI inaendelea kuliratibu hili na kupokea maoni ili kuweza sasa kuelekea kwenye kufanya mabadiliko na kuboresha namna ya kuweza kuutoa mfuko huu na kuhudumia wananchi wetu.

Mheshimiwa Spika, ninaomba kuwasilisha.

Name

Fadhili Sandali Chilombe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kusini

Primary Question

MHE. KASSIM HASSAN HAJI aliuliza: - Je, lini Serikali italeta narekebisho ya sheria ili kuondoa changamoto zinazoendelea katika utekelezaji wa Mfuko wa Jimbo?

Supplementary Question 2

MHE. ENG. FADHILI S. CHILOMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwanza ninaishukuru na kuipongeza Serikali kwa uamuzi wake wa kutoa mfuko huu kwa ajili ya maendeleo ya majimboni kwetu.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa ninaomba kujua kwamba kwa kuwa wakati wa uamuzi huu ulipokuwa unafanyika ni tofauti na sasa, kwamba hali ya maisha imepanda na gharama za vitu zimeongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali haioni haja sasa ya kuongeza kiwango cha fedha inayopelekwa majimboni ili kutuwezesha kupambana hali tuliyonayo? (Makofi)

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Fadhili kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI kama nilivyosema awali tunaendelea kupokea maoni na haya ni maoni ambayo Mheshimiwa Fadhili ameyatoa na Wabunge wengi humu ndani wameendelea kutoa maoni hayo na sisi tupo tayari kuendelea kuyafanyia kazi maoni hayo na pindi itakapokuwa tayari, Serikali itakuja mbele ya Waheshimiwa Wabunge kuwaambia nini tumefanya na nini kimeongezeka ili kuweza kuboresha mfuko huu na ukalete tija kwenye majimbo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KASSIM HASSAN HAJI aliuliza: - Je, lini Serikali italeta narekebisho ya sheria ili kuondoa changamoto zinazoendelea katika utekelezaji wa Mfuko wa Jimbo?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwa kuwa Serikali imesema italeta marekebisho ya sheria ya kuhusu Mfuko wa Jimbo na tunajua kabisa kwamba Wabunge wote humu ndani tunahaki sawa na tunafanya kazi kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, haioni kwamba katika kurekebisha sheria hizo ikawa-include Wabunge wa Viti Maalum kwenye Mfuko wa Jimbo kwa sababu na wenyewe wanafanyakazi kwa wananchi? (Makofi)

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Christina Mnzava, Mbunge wa Mkoa wa Shinyanga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema awali tayari Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI tumeanza kuratibu kwa kupokea maoni haya na nichukue kama maoni maana yake ni swali dogo lakini nichukue kama maoni kwamba tuwa-accommodate kwenye namna ya kwenda kufanyia mabadiliko ili sasa kuona namna gani mfuko huu tutaweza kuutanua na ili Wabunge waweze kuwa na nguvu kule majimboni kuweza kupitia miradi ambayo imekwama waweze kuikwamua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.