Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 27 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 307 | 2026-05-12 |
Name
Prof. Joyce Lazaro Ndalichako
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Kasulu Mjini
Primary Question
MHE. PROF. JOYCE L. NDALICHAKO aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua changamoto ya uhaba wa Watumishi wa Kada ya Afya katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA
SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Prof. Joyce Lazaro Ndalichako, Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini, kama
ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka 2020/2021 hadi mwaka 2025/2026 jumla ya watumishi wa kada za afya 37,921
wameajiriwa na kupangiwa vituo vya kazi katika Mamlaka za Serikali
za Mitaa. Halmashauri ya Mji Kasulu ina mahitaji ya watumishi wa Kada za afya 868 waliopo ni 343, sawa na 40% na upungufu ni
watumishi 525 sawa na 60%.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2025/2026 Serikali imeajiri
jumla ya wataalam wa kada za afya 5,000 na kuwapanga katika
Halmashauri zenye upungufu, ikiwemo Halmashauri ya Mji wa Kasulu
iliyopangiwa watumishi 31.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga bajeti na kuajiri wataalam wa kada mbalimbali za Afya na kuwapanga katika halmashauri zenye upungufu nchini ikiwemo Halmashauri ya Mji wa
Kasulu, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved