Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Prof. Joyce Lazaro Ndalichako

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kasulu Mjini

Primary Question

MHE. PROF. JOYCE L. NDALICHAKO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua changamoto ya uhaba wa Watumishi wa Kada ya Afya katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu?

Supplementary Question 1

MHE. PROF. JOYCE L. NDALICHAKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza, ninapenda kuishukuru Serikali kwa majibu, lakini pia, ninapenda kushukuru kwa watumishi 31 ambao walipangiwa ajira katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika majibu Mheshimiwa Naibu Waziri amekiri kwamba, mahitaji ya watumishi wa afya katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu ni watumishi 525, yaani sawa na upungufu wa 60%.
Upungufu huo unaathiri utoaji wa huduma katika Hospitali ya Mlimani, Kituo cha Afya Kiganamo, Heru Juu pamoja na Nyansha na pia katika zahanati zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu kwa Serikali, je, kwa kuzingatia upungufu wa 60% ya watumishi wa kada za afya katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Serikali ipo tayari katika ajira nyingine kutupangia watumishi wengi zaidi, ili waende kuimarisha huduma za utoaji wa afya? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili. Hawa watumishi ambao tumepangiwa baadhi yao wameshaanza kupata uhamisho kwenda katika maeneo mengine. Je, Serikali iko tayari kuweka mfumo ambao watumishi wanapokuwa wanahama, basi tunapata watumishi mbadala, ili waweze kuendelea kutoa huduma za afya? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ninampongeza sana Mheshimiwa Prof. Joyce Lazaro Ndalichako, Mbunge wa Kasulu, amekuwa mfuatiliaji wa karibu sana wa watumishi wa sekta mbalimbali, ikiwemo sekta ya afya, katika Jimbo la Kasulu Mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watumishi wameendelea kuhitajika katika maeneo mbalimbali kote nchini, na moja ya sababu ya mahitaji makubwa ya watumishi ni kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Serikali hii ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kujenga vituo vya afya kwa
wingi zahanati, hospitali za wilaya na automatically imeongeza uhitaji wa watumishi, lakini Serikali imekuwa ikitoa kibali cha ajira kila mwaka. Hivi karibuni katika siku zile 100 za kwanza za Serikali hii ya Awamu ya Sita kipindi cha pili imeajiri watumishi wa sekta ya afya 5,000 na kuwapanga kwenye maeneo yenye uhitaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeweka utaratibu, tumeainisha mikoa yote na halmashauri zote zenye upungufu zaidi wa watumishi na wakati wa vibali vya ajira halmashauri hizi, ikiwemo Halmashauri ya Kasulu Mjini, zinapewa kipaumbele kwa kupelekewa watumishi wengi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Prof. Ndalichako kwamba, Halmashauri ya Kasulu ni miongoni mwa halmashauri ambazo zimeainishwa kwenye halmashauri zenye upungufu mkubwa wa watumishi na itaendelea kupewa kipaumbele kupelekewa watumishi wengi zaidi kila kibali kinapotokea kuhakikisha kwamba tunapunguza gap la watumishi katika eneo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili, kuhusu uhamisho wa watumishi. Katika ajira zinazotolewa na Serikali tumeweka masharti kwamba, mtumishi yeyote anayepangiwa kwenye kituo hatakiwi kuhama, angalau ndani ya miaka mitatu baada ya kupangiwa kituo kile, isipokuwa kama ana sababu nzito za kiafya na zile ambazo Serikali itajiridhisha kwamba asaidiwe kwa uhamisho. Kwa hiyo, tutaendelea kuhakikisha tunasimamia suala hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, yako maeneo ambayo watumishi wamehamishwa kila tunapoajiri. Tutaendelea kuona tunafanya msawazo wa ndani, lakini pia kupeleka watumishi wengine katika maeneo haya, ahsante. (Makofi)

Name

Nuru Issa Kashakari

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kusini

Primary Question

MHE. PROF. JOYCE L. NDALICHAKO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua changamoto ya uhaba wa Watumishi wa Kada ya Afya katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu?

Supplementary Question 2

MHE. NURU I. KASHAKARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Uvinza ina vituo vya afya viwili ambavyo vinahudumia wananchi. Kwa mfano, Kituo cha Afya Nguruka na Ilagala; Kituo cha Afya cha Nguruka kinahudumia zaidi ya wananchi 362,000, na Kituo cha Afya cha Ilagala kina hudumia wananchi 163,000. Pale kuna uhaba wa watumishi, watumishi ni wachache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupita wananchi wanaohudumiwa katika vituo hivi, je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka watumishi wa afya kwenye maeneo haya ili kuwasaidia wananchi? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba, katika Halmashauri ya Uvinza tuna hicho
Kituo cha Afya cha Nguruka ambacho kwa kweli kiko katikati ya mji na kinahudumia wananchi wengi sana, na Serikali imeendelea kupeleka fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamhakikishia tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatambua tunahitaji kupeleka watumishi zaidi katika Kituo hiki cha Afya cha Nguruka na pia, cha Ilagala, ili kuboresha huduma. Tutahakikisha kila kibali cha ajira kinapojitokeza tunawapa kipaumbele katika vituo hivi vya afya na vingine vyewe upungufu wa watumishi, ahsante sana. (Makofi)

Name

Neema Peter Majule

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. PROF. JOYCE L. NDALICHAKO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua changamoto ya uhaba wa Watumishi wa Kada ya Afya katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. NEEMA P. MAJULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kumwuliza Naibu Waziri kwamba, Mkoa wa Dodoma una kata 209 na vijiji 844. Serikali imejitahidi sana kujenga hospitali, vituo vya afya na zahanati, lakini tukifanya kampeni tumepita, zahanati nyingine zina mtumishi mmoja na nyingine watumishi wawili, na hivyo, imelazimika
wanawake wa Dodoma wanaotaka kujifungua kwenye sehemu husika kusafiri, tena muda mrefu kwa ajili ya huduma ya kujifungua. Mheshimiwa Naibu Waziri, ni lini vituo hivi ambavyo mmejua kabisa vimejengwa vitapata watumishi? Ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba tunavyo vituo vya afya vingi katika Mkoa
wa Dodoma, kama Mheshimiwa Dkt. Neema, alivyosema. Dhamira ya Serikali ni kusogeza karibu zaidi na wananchi huduma za afya, ili kuwapunguzia umbali wa kupata huduma hizo wananchi wengine
wakiwepo akina mama wajawazito. Tufahamu kwamba vipo vituo ambavyo vina upungufu wa watumishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kwanza ambalo Serikali imehakikisha inalisimamia kwa karibu ni kwamba, vituo vyote vilivyojengwa vianze kutoa huduma hata kama kuna watumishi wachache. Tuhakikishe wajawazito na wananchi wengine
wanaendelea kupata huduma, wakati tunaendelea kujipanga kupeleka watumishi wengine katika vituo hivi.