Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 44 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 519 | 2026-06-05 |
Name
Hamoud Abuu Jumaa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibaha Vijijini
Primary Question
MHE. HAWA M. CHAKOMA K.n.y. MHE. HAMOUD A. JUMAA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Barabara ya Kongowe - Soga kwenye station ya Soga kwa kiwango cha lami?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Hamoud Abuu Jumaa, Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa ujenzi wa Barabara ya Kongowe – Soga yenye urefu wa jumla kilometa 17.5, kwani itarahisisha usafiri na usafirishaji kwa wananchi watakaotumia huduma za treni, kupunguza msongamano wa magari, pamoja na kuboresha barabara zinazohudumia shughuli za viwanda ambapo kwa sasa imeanza kufanyiwa usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mara baada ya usanifu kukamilika na gharama halisi za utekelezaji kufahamika, Serikali itatenga fedha kwa ajili ya ujenzi, lakini katika mwaka wa fedha 2023/2024, shilingi milioni 500 zilitumika kuboresha Barabara ya Kongowe–Soga jumla ya kilometa nane kwa kiwango cha changarawe. Kazi zilizotekelezwa zilijumuisha ujenzi wa makalavati, uchimbaji na ujenzi wa mitaro ya maji, pamoja na kuziba mashimo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka wa fedha 2025/2026 jumla ya shilingi milioni 44.2 zimetengwa kwa ajili ya kufanya matengenezo ya Barabara ya Kongowe – Soga kilometa nane. Aidha, Serikali imeweka katika mpango wa mwaka 2026/2027 ujenzi wa sehemu korofi kwa gharama ya shilingi milioni 279.9
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuihudumia barabara hii kwa matengenezo, ujenzi na ukarabati kulingana na upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved