Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Hawa Mchafu Chakoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAWA M. CHAKOMA K.n.y. MHE. HAMOUD A. JUMAA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Barabara ya Kongowe - Soga kwenye station ya Soga kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 1
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali na naomba niulize maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Waziri pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninachotaka kufahamu, kwa kuwa barabara hiyo iko katika hatua ya usanifu kama ambavyo umesema na kwa kuwa barabara hiyo ni muhimu sana kwa namna vile ulivyosema inatuunganisha na stesheni ya SGR, lakini pia kuna Kiwanda kikubwa cha Nyama cha Tanchoice ambacho kinafanya biashara kubwa sana kule na kwa kuwa barabara ile haipitiki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni upi mpango wa muda mfupi wa Serikali ili kuhakikisha huduma inaendelea kupatikana kama ilivyokuwa awali?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, kwa kuwa umesema barabara ile ina kilometa 16.5 tu, ni kwa nini sasa barabara hii isitoke kwa TARURA na ikaenda kwa TANROADS kwa umuhimu wa barabara hii? Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali madogo ya nyongeza ya Mheshimiwa Hawa kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa Serikali mfupi wa kuhakikisha barabara hii tuna ihudumia na tunairudisha katika hali yake, kwa kutumia Bunge lako Tukufu hili nimuelekeze Meneja wa TARURA Wilaya afike katika maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyaainisha kufanya tathmini na kutuletea andiko Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI na kuona namna gani tutachukua hatua za dharura ili kuweza kufanikisha miundombinu hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ni jibu kwa ujumla, mtaona kwamba kuanzia mwaka 2020 mpaka 2021, bajeti yetu ya TARURA ilikuwa wastani wa shilingi bilioni 275 lakini mpaka leo hii, mwaka 2026/2027 tumetenga zaidi ya shilingi bilioni 871 ambalo ni ongezeko la zaidi ya mara tatu ya kile ambacho tulikuwa tukikitekeleza mwaka 2021.
Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge pamoja na Wabunge wengine kwamba tunaenda kuongeza nguvu katika TARURA na kuweza kuzihudumia barabara zetu hizi, ninaomba kuwasilisha.
Name
Subira Khamis Mgalu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAWA M. CHAKOMA K.n.y. MHE. HAMOUD A. JUMAA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Barabara ya Kongowe - Soga kwenye station ya Soga kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 2
MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwa kuwa Serikali mwaka 2025 kupitia Waziri wa TAMISEMI, iliahidi kutoa kiasi cha shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwenye Kata ya Kerege, kuelekea eneo la viwanda, ambako moja ya kiwanda kilichopo ni cha kuunganisha magari, kiwanda cha pekee Afrika Mashariki ya Kati. Je, ni lini Serikali itatimiza ahadi hii kwa ajili ya Kata ya Kerege? (Makofi)
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ninaomba kujibu swali la nyongeza kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameliuliza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba ahadi za Serikali tutazitimiza kwa kadri ambavyo tunavyopokea bajeti. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa maeneo ya barabara ambayo ameyaainisha, tutaendelea kutenga fedha ili kutekeleza ahadi hizo ili kuendelea kutoa huduma ambayo Serikali imekusudia katika maeneo hayo, ninaomba kuwasilisha.
Name
Hawa Subira Mwaifunga
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAWA M. CHAKOMA K.n.y. MHE. HAMOUD A. JUMAA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Barabara ya Kongowe - Soga kwenye station ya Soga kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 3
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kuniona.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Mbugani, barabara nyingi hazipitiki na ni mbovu, zina mashimo mengi. Barabara ya Kamna – Tandale – Sekulu - Mzaganza – Usule - Miembemingi na Tandale mpaka Kiwanda cha Nyuzi; barabara hizi zina hali mbaya na mvua ziliponyesha kuna mashimo makubwa kiasi kwamba wananchi wanashindwa kufanya shughuli zao kwa sababu ya ubovu wa barabara.
Nini kauli ya Serikali juu ya kufanya ukarabati wa barabara hizi, angalau mtujengee kwa kiwango cha changarawe ili wananchi hawa wa Kata ya Mbugani waweze kupata tabasamu?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hawa Mwaifunga, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa swali ambalo ameliuliza na mimi huwa ninapita njia ile ya Tabora, kwa hiyo, huwa nyingi huwa zinaathiri sana ule mji wetu wa Tabora.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumhakikisha tu Mheshimiwa Hawa Mwaifunga, sasa mvua zile za masika zinaelekea ukingoni na bajeti ya TARURA imeongezeka maradufu, ukiangalia kutoka mwaka 2021 mpaka leo imeongezeka zaidi ya mara tatu.
Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Hawa Mwaifunga, tutatenga bajeti kwa ajili ya kurekebisha barabara hizi kwa kiwango cha changarawe ili ziendelee kutoa huduma katika jimbo lake na wananchi waendelee ku-enjoy tabasamu la Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ninaomba kuwasilisha.
Name
Jonas William Mbunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbinga Mjini
Primary Question
MHE. HAWA M. CHAKOMA K.n.y. MHE. HAMOUD A. JUMAA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Barabara ya Kongowe - Soga kwenye station ya Soga kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 4
MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Mbinga - Mbangamao hadi Mpepai kilometa 32 imeharibiwa sana na mvua katika kipindi kirefu. Ni lini Serikali itafanya mkakati wa kuhakikisha kwamba barabara hiyo inatengenezwa?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyingeza la Mheshimiwa Mbunge kama ambavyo ameliuliza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI tulifanya tathmini ya barabara zote nchini na hadi kufukia barabara zote za wilaya ambazo zinahudumiwa na TARURA mpaka sasa tuna jumla ya kilometa 47,000 na zaidi ya kilometa 47,000 ambayo ni sawasawa na zaidi ya 32.9% ambazo zina hali mbaya nchini na barabara hizi zinahitaji jumla ya shilingi bilioni 264 kufanyiwa marekebisho zirudi katika hali yake.
Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa sababu tunaelekea mwisho wa msimu wa mvua tutatenga bajeti kwa ajili ya matengenezo ya barabara hizo ili ziendelee kupitika na kutoa huduma kwa wananchi, ninaomba kuwasilisha.
Name
Zuberi Yahya Mfaume
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Morogoro Kusini
Primary Question
MHE. HAWA M. CHAKOMA K.n.y. MHE. HAMOUD A. JUMAA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Barabara ya Kongowe - Soga kwenye station ya Soga kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 5
MHE. ZUBERI Y. MFAUME: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza swali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Kata ya Bwakira Juu inayounganisha na Kata ya Bwakira Chini, barabara hii sasa haipitiki, sio tu kwa gari, hata kwa pikipiki. Je, ni lini sasa Serikali itafanya ukarabati wa barabara hii ili iweze kupitika?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zuberi Mfaume, kama alivyoliuliza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu kwenye majibu yangu ya awali, Mkoa wa Morogoro unafahamika kijiografia unapokea maji mengi sana kutoka mikoa mingine kutoka Manyara, kwa hiyo, zile barabara zinaharibika hata kama mvua hazinyeshi katika Mkoa wa Morogoro.
Kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge, pamoja na wananchi ambao wanawahudumia, TARURA tutaendelea kutengea bajeti ili kurekebisha barabara hizi, ninaomba kuwasilisha.
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. HAWA M. CHAKOMA K.n.y. MHE. HAMOUD A. JUMAA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Barabara ya Kongowe - Soga kwenye station ya Soga kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 6
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, sijajua sasa kitu gani kinatokea katika Wilaya, Jimbo la Bunda; wakandarasi wote wamesimama kwa sababu hawana fedha. Sasa ni lini mtawalipa wakandarasi wa Bunda ili waendelee na barabara zao?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Getere, kama alivyoliuliza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekwishafanya tathmini katika wilaya zote nchini na tumekwishaandaa mpango, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, kama nilivyosema zaidi ya bilioni 264 zinatakiwa ili ziende kwa wakandarasi wetu waweze kutengeneza barabara hizi.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Getere nikuhakikishie, tutakapotenga bajeti Serikali tutakupa taarifa ili tuhakikishe kwamba unakwenda kuzisimamia fedha hizi kwa wakandarasi hawa ili wazijenge barabara hizi kwa kiwango kinachotakiwa, ninaomba kuwasilisha.