Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 44 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 520 | 2026-06-05 |
Name
Bakari Bakari Shingo
Sex
Male
Party
ACT
Constituent
Ukonga
Primary Question
MHE. BAKARI B. SHINGO aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa Barabara ya Pugu – Mnadani – Bangulo hadi Ulongoni B utaanza?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Bakari Bakari Shingo, Mbunge wa Jimbo la Ukonga kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Pugu – Mnadani – Bangulo hadi Ulongoni B ina urefu wa jumla ya kilometa 4.36 ambapo imetengewa jumla ya shilingi bilioni 2.017 kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami urefu wa kilometa 1.2.
Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa ujenzi huu unafanyika kwa awamu mbili; awamu ya kwanza ni urefu wa kilometa 0.3 kwa gharama ya shilingi milioni 575.526 kupitia chanzo cha mapato ya ndani ya halmashauri na ujenzi wa awamu ya pili una urefu wa kilometa 0.9 kwa gharama ya shilingi bilioni 1.442 kupitia fedha za jimbo na tozo za mafuta.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa awamu ya kwanza umekamilika, kwa sasa mkandarasi anaendelea na Ujenzi wa awamu ya pili, ambapo utekelezaji wake umefikia 10%.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuhudumia mtandao wa barabara wa Jimbo la Ukonga kwa kujenga, kufanya ukarabati na Matengenezo kulingana na upatikanaji wa fedha, ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved