Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 44 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 522 | 2026-06-05 |
Name
Sikudhani Yasini Chikambo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO aliuliza:-
Je, lini Serikali itamlipa mkandarasi ili kukamilisha Mradi wa Maji Tunduru ambao umesimama?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sikudhani Yassini Chikambo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji unaolenga kunufaisha Mji wa Tunduru unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 3.4. Mradi huo upo kwenye hatua za awali za utekelezaji ambapo unahusisha ujenzi wa dakio, ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 1,000,000 sanjari na ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 98.7.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali tayari imepeleka jumla ya shilingi 511,327,133.14 ikiwa ni fedha za malipo ya awali kwa maana ya advance payment kwa mkandarasi na wazabuni wanaohusika katika utekelezaji wa mradi huo. Hivyo, ninamwelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tunduru kuharakisha uratibu wa malipo kwa wahusika ndani ya siku saba kuanzia leo.
Aidha, nimtake mkandarasi kurejea eneo la kazi ili kuendelea na utekelezaji wa mradi huo unaolenga kunufaisha zaidi ya wananchi 75,674 wa Mji wa Tunduru na viunga vyake, ninakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved