Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 44 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 523 2026-06-05

Name

George Natany Malima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Daraja la Godegode kwa kuwa mkandarasi ameshapatikana?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa George Natany Malima, Mbunge wa Mpwapwa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, taratibu za manunuzi ya kumpata mkandarasi wa ujenzi wa Daraja la Godegode zimekamilika. Kwa sasa tunaendelea kutafuta fedha za malipo ya awali (advance payment) ili mkataba usainiwe na kazi ya ujenzi ianze, ahsante.