Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 44 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 524 | 2026-06-05 |
Name
Husna Juma Sekiboko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: -
Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Lushoto, Magamba, Lukozi, Mlalo mpaka Umba Junction kwa kiwango cha lami?
Name
Abdallah Hamis Ulega
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkuranga
Answer
WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Husna Juma Sekiboko, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Lushoto – Magamba – Lukozi – Mlalo hadi Umba Junction kilometa 66.35, ni barabara inayohudumiwa na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Tanga. Kwa sasa Serikali inaendelea na maandalizi ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hii ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami. Baada ya hatua hiyo kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha za ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved