Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Husna Juma Sekiboko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Lushoto, Magamba, Lukozi, Mlalo mpaka Umba Junction kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwanza nishukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Waziri, lakini nimshukuru sana Waziri Mkuu Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, wakati wa ziara yake katika Jimbo la Mlalo alitoa maelekezo barabara hii kujengwa yote kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ujenzi wa barabara hii upembuzi yakinifu na usanifu wa kina unachukua muda kama ambavyo Mheshimiwa Waziri ameeleza hapo; kwanza, wafanye upembuzi na baadaye itafutwe fedha kwa ajili ya ujenzi.

Sasa wakati hayo maandalizi yote yanafanyika, kwa nini Serikali isi-release, isitoe fedha ili kuendelea kutekeleza ule ujenzi wa vipande vipande kama ilivyokuwa awali?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, barabara hii pia ina mzunguko wa kutoka Magamba kwenda Lukozi – Mlalo, lakini mzunguko mwingine ni kutoka Lukozi kupita Manolo kwenda Sunga - Mtae mpaka Lunguza ambapo inakutana na hii Umba Junction.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuijenga pia barabara hii ya mzunguko wa juu kupitia Mtae kwenda Umba Junction kwa kiwango cha lami? (Makofi)

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza, ninashukuru kwa maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Husna Sekiboko, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Tanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninafahamu matamanio ya Mheshimiwa Mbunge ni kuona hatua hizi zote zinakamilika kwa haraka na ujenzi wa kiwango cha lami ambao utawaondolea adha wananchi wa kutoka Lushoto na Mlalo wapate nafuu. Lushoto na Mlalo ambapo Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Profesa Riziki Shemdoe na Mbunge wa Mlalo Mheshimiwa Rashid Shangazi wamekuwa wakiipigania sana barabara hii wakati wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka nimhakikishie tu kwamba ameniomba wakati tunaendelea na hatua hizi ule utaratibu wa kutazama walau vipande vidogo vidogo uendelee.

Sasa ninampa comfort kwamba nimeelekeza wataalam wangu waniletee nitoe idhini ya kipande cha kilometa 2.4 cha kutoka Nyasa mpaka Majulai katika Jimbo la Mlalo ambalo linawakilishwa na Mheshimiwa Rashid Shangazi, tutahakikisha kwamba tunakwenda kumtafuta mkararasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kwa kuwa uelekeo wetu mara baada ya bajeti kuu kupita Wakala wetu wa Mfuko wa Barabara Tanzania tunatarajia mambo yatakwenda kuwa mazuri na kwa hiyo, tutafanya kazi ya kutengeneza vipande vile ambavyo vinaonekana ni korofi na sumbufu kwa wananchi ikiwa ni pamoja na Jimbo hili la Mlalo na kule Lushoto kama nilivyotamka mwanzo kutoka Nyasa kwenda Majulai tutawapa kipaumbele kwa mzingatio huu wa Mheshimiwa Husna Sekiboko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ameniuliza kuhusiana na kipande ambacho hakizungumzwi cha kuelekea Mtae mpaka Umba Junction na Umba Junction mpaka Mkomazi barabara ambayo inaunganisha na Wilaya ya Same ni barabara muhimu sana. Sasa kwa hiki kipande cha kuelekea Mtae ninatoa maelekezo kwa wataalam wetu wa TANROADS hususani wa Mkoa wa Tanga na chenyewe wakianzie kazi maana kile cha kwenda Magamba kuunganisha na Wilaya ya Mkinga chenyewe tayari kama nilivyojibu katika swali la awali. Kinakwenda vizuri. Sasa tutaelekeza fikra yetu pia upande wa kuelekea Mtae.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimpe uhakika Mheshimiwa Husna Sakiboko na Wanatanga na majirani zao pia vilevile wa upande wa Same - Kilimanjaro kwamba tumelichukuchukua jambo hili na kuitazama barabara ya kuelekea Mtae ili tuweze kuianzia hatua kwa hatua kama ambavyo ile ya kuelekea Magamba tumeipa kipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.

Name

Adonis Alfred Bitegeko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba Kaskazini

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Lushoto, Magamba, Lukozi, Mlalo mpaka Umba Junction kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 2

MHE. ADONIS A. BITEGEKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kunipa nafasi kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Muleba, Jimbo la Muleba Kaskazini kuna barabara za kutoka Kamachumu Center kwenda Hospitali ya Ndolage na kutoka Kata ya Nshamba kwenda Kata ya Mushabago katika Kijiji cha Rushwa ambazo tayari zimeshafanyiwa usanifu na TANROADS zinasubiri kujengwa kwa kiwango lami. Je, ni lini Serikali itaanza kujenga barabara hizo?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nijibu swali hili la wananchi wa Muleba kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimechukua na ninashukuru kwamba hatua ya usanifu imekwisha kupita. Nitoe tu maelekezo kwa Meneja wetu wa TANROADS wa Mkoa wa Kagera, Engineer Joel aweze kuhakikisha kwamba hatua za awali ikiwa ni pamoja na kuileta sasa upande wa headquarter ya TANROADS na Wizarani ili tuweze kuitafutia fedha na ili tuweze kuitengeneza barabara hii ya wananchi inayoanzia pale Kamachumu kwa kiwango hiki cha lami pindi upatikanaji wa fedha utakapokuwa mzuri. Ahsante sana.

Name

Agnesta Lambert Kaiza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Lushoto, Magamba, Lukozi, Mlalo mpaka Umba Junction kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 3

MHE. AGNESTA L. KAIZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara kutoka Kifuru kuelekea Pugu Station - Mnadani ni barabara ambayo ipo ndani ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi tangu enzi za Hayati Magufuli, na hivi sasa ninavyoongea barabara hii ni mbovu na nimekuwa nikiongea na wewe na umekuwa ukinipa ushirikiano mkubwa sana, ninakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali langu, ni lini barabara hii mtakwenda kuijenga kwa sababu wananchi wanapata adha kubwa na mifugo inapata adha kubwa kuelekea Pugu Mnadani. Mheshimiwa Waziri, ninaomba tabasamu kwa Wana-Kifuru kuelekea Pugu Station. Na nikuombe ukubali kuambatana na mimi baada ya Bunge hili uende kujionea hali halisi jimboni kwangu. Ahsante sana.

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na nashukuru kwa swali la nyongeza la Mheshimiwa Agnesta Lambert, Mbunge wa Jimbo la Segerea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninakubali ombi la kwenda kuambatana naye kuelekea Segerea kwenda kukagua miundombinu ya Jimbo la Segerea. Niko tayari mara baada ya Mkutano huu wa Bajeti kukamilika tutafanya ziara na niwape comfort watu wa Segerea, ninafahamu barabara zao nyingi zimepondwapondwa na zimeharibika wakati huu wa mvua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana Naibu Waziri wa TAMISEMI na Waziri wa TAMISEMI pia ambapo barabara hizi nyingi zinaangukia upande wa TARURA, lakini wamezipangia mpango mzuri. Tuna mradi mkubwa kule wa DMDP II ambao Mheshimiwa Agnesta na Wabunge wengine wa Mkoa wa Dar es Salaam wamekuwa wakiufuatilia kwa karibu sana na kuusisitiza sana. Ninaamini kwa uelekeo huo, Dar es Salaam inakwenda kubadilika kwa kiwango kikubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Agnesta na wana-Dar es Salaam pia msisahau barabara ile ya Mandela kuanzia Ubungo kwenda bandarini tunakwenda kujenga barabara ya kisasa inayounganishwa na mwendokasi, lakini pale junction ya Tabata tutajenga flyover ili pawe na urahisi na kutoleta msongamano katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tukienda Kifuru – Pugu Mnadani, ni kweli kwamba barabara ile ni mbovu na ni barabara muhimu kwa ajili ya watu kwenda kuungana kwenda kupanda treni yetu ya kisasa ya SGR.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwape comfort Wabunge wote, kwenye maeneo ambayo yana vituo vyetu vya SGR, mkakati wetu ndani ya Serikali ni kuhakikisha tunafungamanisha. Sisi Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi tunazungumza lugha moja ili watu wapate urahisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimefurahi pia asubuhi ya leo nimesikia maswali ya namna hii ikiwa ni pamoja na lile swali la kwetu pale Pwani la kutoka Mlandizi kwenda Ruvu Station ambayo tayari mkandarasi tumekwishampata wakati wowote tutamlipa advance payment.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, kule Tabora kwa Mheshimiwa Bashungwa na Mheshimiwa Luhende wamekuwa wakipigania sana barabara ya kutoka Nzega – Bukene ambayo inakwenda kuwaunganisha na station ya SGR. Mheshimiwa Bashe amekuwa akihangaika sana na jambo hili muda mrefu na nataka niwape comfort ya kwamba tumezungumza na wenzetu wa Wizara ya Uchukuzi tunakwenda kuijenga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale Pugu Station ng'ombe wanavunjika miguu kwenye malori kwa sababu ya kipande kile tu. Ni msisitizo wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kwamba tunajenga barabara hizi na tutazijenga, si tu kwa sababu ya kujenga kwa sababu ya kupata idadi kubwa ya viwango vya lami, lakini ni kwa kuzingatia tabasamu la utu kwa Watanzania. Tutafanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa na uaminifu ili Watanzania waweze kupata huduma iliyo bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakupongeza tena Mheshimiwa Agnesta kwa upambanaji wako wewe na Wabunge wote wa Mkoa wa Dar es Salaam, ni kazi nzuri mnayoifanya, nina hakika tutakwenda kuibadilisha Dar es Salaam na itapendeza sana. (Makofi)