Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 44 | Industries and Trade | Wizara ya Viwanda na Biashara | 525 | 2026-06-05 |
Name
Janeth Elias Mahawanga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza: -
Je, BRELA inachukua hatua gani kulinda bidhaa za wanawake dhidi ya wizi wa nembo, chapa au mawazo ya ubunifu?
Name
Dennis Lazaro Londo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mikumi
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, naomba sasa nijibu swali namba 525 kama lilivyoulizwa na Mheshimiwa Janeth Elias Mahawanga, Mbunge wa Viti Maalum.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia BRELA imekuwa ikilinda bidhaa za wafanyabiashara wakiwemo wanawake dhidi ya wizi wa nembo, chapa na mawazo ya ubunifu kupitia usajili wa alama za biashara na huduma kwa mujibu wa Sheria ya Alama za Biashara na Huduma, Sura Namba 326.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria hii inampa mmiliki haki ya kipekee ya kutumia alama hiyo na kumwezesha kuchukua hatua za kisheria endapo itatumiwa bila idhini yake. Usajili wa alama hizo hufanyika kupitia mfumo wa mtandaoni wa usajili wa BRELA ambao unatambulika kama Online Registration System.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved