Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Janeth Elias Mahawanga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza: - Je, BRELA inachukua hatua gani kulinda bidhaa za wanawake dhidi ya wizi wa nembo, chapa au mawazo ya ubunifu?
Supplementary Question 1
MHE. JANETH E. MAHAWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Pamoja na majibu hayo, nina maswali madogo mawili ya nyongeza.
Swali la kwanza, kwa kuwa wanawake wengi wanajishughulisha na shughuli za utengenezaji wa bidhaa za chakula, vipodozi na kazi za mikono, je, Serikali imejipangaje kuhakikisha inazilinda bidhaa hizi dhidi ya bidhaa zinazotumia chapa fake kwa ajili ya wajasiriamali hawa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, BRELA imejipangaje kuhakikisha wanawake wa vijijini wanafikiwa na huduma za chapa na alama za biashara? (Makofi)
Name
Dennis Lazaro Londo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mikumi
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza natumia nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Janeth Mahawanga kwa jitihada zake ambazo zimekuwa mkombozi mkubwa kwa wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia BRELA tumekuwa tukitoa elimu kwa wanawake wajasiriamali na kwa mwaka jana pekee tumewafikia wanawake zaidi ya 1,000 katika mikoa 13 ya Tanzania Bara. Mikoa hiyo ni Shinyanga, Morogoro, Songwe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Pwani, Dodoma, Geita, Simiyu, Manyara na Mara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunawafikiaje wanawake hasa wa vijijini? Shirika la BRELA kwa kushirikiana na SIDO wamekuwa wakiendesha mafunzo kwa wajasiriamali kwa ajili ya kulinda bunifu, lakini kuwaelezea umuhimu wa usajili wa alama za biashara na mawazo ama bunifu mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo, BRELA imekuwa ikishiriki matukio mbalimbali kama Sabasaba, Nanenane na maonesho ya taasisi mbalimbali ikielimisha wajasiriamali katika maeneo tofauti ya nchi, lakini pia imekuwa ikitoza usajili wa hapo kwa papo na kazi hii imekuwa ikifanyika katika mikoa mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi la Mheshimiwa Mbunge ni kufika katika Mkoa wa Dar es Salaam na naomba kutumia nafasi hii kumpa faraja Mheshimiwa Mbunge kwamba kuna maelekezo kwa BRELA kuanza kutoa elimu hii katika maeneo ya pembezoni mwa Mkoa wa Dar es Salaam na kazi hii imeshaanza na inaendelea. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Name
Mariam Madalu Nyoka
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza: - Je, BRELA inachukua hatua gani kulinda bidhaa za wanawake dhidi ya wizi wa nembo, chapa au mawazo ya ubunifu?
Supplementary Question 2
MHE. MARIAM M. NYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru; je, Serikali ina mfumo gani wa kufuatilia na kubaini chapa zinazokiuka hakimiliki za watu wengine kabla ya kusajiliwa? (Makofi)
Name
Dennis Lazaro Londo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mikumi
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Sheria ya Alama za Biashara na Huduma, Sura Namba 326 ni kosa kutumia alama za biashara ama miliki bunifu za mtu. Kwa hiyo, elimu ambayo tumekuwa tukiitoa ni kuwaomba wajasiriamali mbalimbali kusajili kwanza miliki bunifu zao, lakini kutupa ushirikiano pale wanapoona kwamba kuna watu ambao wanaiba ama wanatumia bila idhini ya hawa wamiliki ambao wamesajili bunifu hizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pale ambapo tunapata taarifa hizo tumekuwa tukishirikiana nao kwa ajili ya kuhakikisha kwamba sheria inachukua mkondo wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Name
Neema Peter Majule
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza: - Je, BRELA inachukua hatua gani kulinda bidhaa za wanawake dhidi ya wizi wa nembo, chapa au mawazo ya ubunifu?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. NEEMA P. MAJULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kumuuliza Waziri; je, Serikali haioni kwamba ni haja sasa ya kuweka wataalam ili wakawasaidie wanawake kubuni hizo alama, halafu na kupunguza gharama waweze kusajiliwa ili wanawake hao watakapokuwa na alama hizo waweze kuhimili ushindani wa soko la nchi za nje? Ahsante. (Makofi)
Name
Dennis Lazaro Londo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mikumi
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu swali la msingi, SIDO wamekuwa wakiendesha madarasa haya kwa kufikia makundi mbalimbali hasa wanawake, kwa mfano, madarasa ya SIDO yanachukua wanafunzi 40 kwa wiki na majority wanakuwa ni wanawake na kwa kuona umuhimu wa kutoa elimu ya kulinda miliki bunifu na alama za biashara, BRELA wamekuwa wakishiriki madarasa haya ya SIDO na ushirikiano huu umekuwa ukizaa matunda kwa maana wanafikia watu wengi na hasa wa pembezoni. Kazi hii inafanyika kwa umakini na matokeo tunayaona.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved