Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 44 Finance Wizara ya Fedha 526 2026-06-05

Name

Tinnar Andrew Chenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TINNAR A. CHENGE aliuliza: -

Je, Serikali inatumia kigezo gani katika kutoza Kodi ya Majengo (Property Tax) kupitia mfumo wa mita za LUKU nchini?

Name

Laurent Deogratius Luswetula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. LAURENT D. LUSWETULA) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tinnar Andrew Chenge, Mbunge wa Viti Maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Serikali inatumia viwango mfuto katika kutoza kodi za majengo kupitia mita za umeme za LUKU. Vigezo vinavyotumika kutoza kodi za majengo kupitia LUKU ni kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja; nyumba ya kawaida ambayo inatozwa shilingi 18,000 kwa mwaka au shilingi 1,500 kwa mwezi; na nyumba ya ghorofa ambayo inatozwa shilingi 90,000 kwa kila sakafu kwa mwaka au shilingi 7,500 kwa kila sakafu kwa mwezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyumba za nyasi, udongo, huduma za jamii, kuabudia na anayoishi wazee kuanzia miaka 60 hazitozwi kodi ya majengo isipokuwa endapo majengo hayo ni ya kibiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.