Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tinnar Andrew Chenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TINNAR A. CHENGE aliuliza: - Je, Serikali inatumia kigezo gani katika kutoza Kodi ya Majengo (Property Tax) kupitia mfumo wa mita za LUKU nchini?

Supplementary Question 1

MHE. TINNAR A. CHENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na nashukuru majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali madogo mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, kwa kuwa kodi hii ya property tax inapaswa kulipwa na mmiliki wa jengo na kwa kuwa kuna wajasiriamali ambao wamepanga kwenye frame za maduka zinazomilikiwa na wafanyabiashara na kwenye frame hizi zimefungwa LUKU. Je, ni kwa nini Serikali inawakata property tax wajasiriamali hawa kwenye mita hizi za LUKU? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; je, Serikali haioni haja kwamba kuna umuhimu sasa wa kuipitia sera hii ili mmiliki wa jengo huyu alipe kodi hii kupitia kwenye mita yake ya LUKU badala ya kumbebesha mzigo mjasiriamali huyu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

Name

Laurent Deogratius Luswetula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. LAURENT D. LUSWETULA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza namshukuru sana Mheshimiwa Tinnar Andrew Chenge na kuendelea kuwapongeza sana wanawake wa Mkoa wa Simiyu kwa kutuletea mtu huyu makini na bora ambaye anajenga hoja za kujenga hapa Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwenye maswali ya nyongeza, yako mawili lakini yenye namna moja ni kama yanashabihiana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kwanza kama Serikali naweze kukiri kabisa, kwa sasa hivi utaratibu unaotumika ndiyo huu ambao Mheshimiwa Tinnar ameuzungumza kwamba inalipwa kupitia LUKU ambapo watumiaji sasa wa LUKU ndiyo wanaolipa. Watumiaji wa LUKU hawa ndiyo wanaweza wakawa ni wamiliki au wanaweza wakawa wapangaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa wapangaji, ndiyo maana tumeliona hili kama Serikali na sisi kwa kushirikiana na wenzetu Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ambapo sasa kwamba hizi halmashauri ziko chini yao, tumekaa na tumechakata na tunaendelea kuchakata kuona namna bora zaidi ambayo sasa tutakusanya kodi hii ya majengo kwa wamiliki na siyo wale wapangaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha. (Makofi)

Name

Zacharia Paulo Issaay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Mjini

Primary Question

MHE. TINNAR A. CHENGE aliuliza: - Je, Serikali inatumia kigezo gani katika kutoza Kodi ya Majengo (Property Tax) kupitia mfumo wa mita za LUKU nchini?

Supplementary Question 2

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, bado kuna haja ya kufanya zoezi hili kwa marejeo katika kipindi fulani fulani kwa ajili ya majengo na matumizi kubadilika mara kwa mara.

Je, Serikali haioni kuwa kuna haja sasa ya kufanya marejeo ya uhakiki wa majengo hayo hasa yale ya wananchi wa makundi ya chini ambayo taratibu zinawataja wasitozwe?

Name

Laurent Deogratius Luswetula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. LAURENT D. LUSWETULA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na ninampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza na mimi nakiri kabisa na nasema ya kwamba kodi hizi za majengo kwa maana ya property tax zinakusanywa na halmashauri kupitia shirika letu la umeme TANESCO ambazo maana yake hizi ni nyumba ambazo zimeunganishwa na umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nyumba ambazo pia hazijaunganishwa na umeme, bado halmashauri zetu zimeendelea kukusanya kwa rate ile ile kulingana na mwongozo unavyotuongoza. Kwa namna hiyo, sisi kama Serikali tumejipanga kabisa na ukiangalia namna mfumo ulivyo, tumejipanga kuhakikisha kwamba halmashauri zetu kwanza zinakusanya kodi hii bila upendeleo, kumpendelea mtu yeyote au nyumba yoyote na ndiyo maana kama mpango wa Serikali kupitia kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, mpaka sasa hivi wale watendaji wetu wa vijiji tumeweza kuwawezesha vishkwambi kwa ajili ya kusajili nyumba ambazo hazijasajiliwa mpaka sasa hivi na hazilipi kodi ya majengo. Tumewawezesha na zoezi hilo linaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hilo, tumewawezesha pia mfumo ambao watakuwa na uwezo wa kutoa control number kupitia vile vishkwambi. Kwa namna hiyo, na mimi natumia fursa hii hii kuwaasa wananchi wote ambao tayari wameshapewa zile control number kuweza kuzilipia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha. (Makofi)

Name

Simon Songe Lusengekile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busega

Primary Question

MHE. TINNAR A. CHENGE aliuliza: - Je, Serikali inatumia kigezo gani katika kutoza Kodi ya Majengo (Property Tax) kupitia mfumo wa mita za LUKU nchini?

Supplementary Question 3

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wamekuwa wakimaliza ujenzi wa nyumba zao baada ya mwaka wa fedha kuwa umeanza, kwa mfano, mwananchi anamaliza kujenga nyumba yake mwezi huu Juni na kuingiza umeme kwa mara ya kwanza lakini amekuwa akikatwa kuanzia mwezi Julai mwaka jana mwaka wa fedha ulivyoanza na kumsababishia madeni ambayo siyo ya msingi kwake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali ina hatua gani kuhakikisha kwamba sasa wananchi wanakatwa kulingana na muda ambao amemaliza ujenzi na kuweka LUKU yake kwenye nyumba yake? (Makofi)

Name

Laurent Deogratius Luswetula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. LAURENT D. LUSWETULA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza nampongeza sana kaka yangu na Mheshimiwa kwa swali lingine zuri kabisa la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nasema tu natumia nafasi hii kusema kwamba mapendekezo yake tumeyapokea kama Serikali. (Makofi)

Name

Fadhili Sandali Chilombe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kusini

Primary Question

MHE. TINNAR A. CHENGE aliuliza: - Je, Serikali inatumia kigezo gani katika kutoza Kodi ya Majengo (Property Tax) kupitia mfumo wa mita za LUKU nchini?

Supplementary Question 4

MHE. ENG. FADHILI S. CHILOMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upo mkanganyiko umekuwa ukijitokeza kwenye majengo mengi na hasa kupitia hii kodi. Unakuta jengo moja labda la ghorofa lina mita zaidi ya tano au 10 au 20 kutegemea na ukubwa wa jengo lenyewe. Mtazamo unaoonekana ni kwamba kila kwenye mita pana nyumba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili limeleta kero kubwa sana kwa wananchi; je, Serikali haioni haja sasa ya kufanya upembuzi yakinifu kuona kwamba ni wapi kuna nyumba, ni wapi hakuna nyumba na nyumba ziko ngapi ili kuondoa kero hiyo kwa wananchi? (Makofi)

Name

Laurent Deogratius Luswetula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. LAURENT D. LUSWETULA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi hii na kwanza, nampongeza sana Mheshimiwa Mbunge na kwa namna alivyotoa hoja yake ni kama anatoa maoni kwa Serikali. Nasema kwamba maoni yake tumeyapokea na tutayafanyia kazi. Ahsante sana. (Makofi)