Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 44 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 527 | 2026-06-05 |
Name
Masache Njelu Kasaka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lupa
Primary Question
MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga mnara katika Kijiji cha Shoga ili kutatua changamoto ya mawasiliano ya simu?
Name
Switbert Zacharia Mkama
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Masache Njelu Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wizara Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inaendelea kuboresha huduma za mawasiliano nchini kwa kutatua changamoto za huduma ya mawasiliano katika maeneo mbalimbali katika Kijiji cha Shoga. Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania kupitia Awamu ya Tisa Mradi wa Mawasiliano Vijijini inaendelea kutekeleza ujenzi wa mnara wa mawasiliano katika eneo la Shoga Pitch ambapo utekelezaji wake unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2026.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 13 Mei, 2026 Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote kwa kushirikiana Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Lupa pamoja na viongozi wa Kijiji cha Shoga ilifanya ziara na kujionea maendeleo ya ujenzi wa mnara huo ambapo mkandarasi, Kampuni ya Huawei Tanzania ameahidi kukamilisha ujenzi ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni, 2026 ili kutatua changamoto ya mawasiliano yaliyopo katika kijiji hicho cha Shoga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved