Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Masache Njelu Kasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupa

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Kijiji cha Shoga ili kutatua changamoto ya mawasiliano ya simu?

Supplementary Question 1

MHE. MASACHE N. KASAKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi, lakini pia ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua nafasi hii kuweza kuipongeza Serikali Kijiji hiki cha Shoga tayari mnara huu wa mawasiliano umeshawaka, na pamoja na mnara huu, na vijiji vingine Kijiji cha Mlemanjiwa, Kijiji cha Igundu, Kijiji cha Mkora, Upendo na Sipa mwezi uliopita wa tano na kwenyewe minara hii ya mawasiliano imewaka. kwa hiyo tunaishukuru sana Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo, nina maswali madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo mengi ya Wilaya ya Chunya ambako ni maeneo ya wachimbaji wadogo yana changamoto kubwa sana ya mawasiliano kiasi kwamba wachimbaji wetu wanapata shida kubwa wanapokuwa maeneo yao ya kazi.

Je, ni upi sasa mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba maeneo haya ya wachimbaji wadogo yanaweza kupata mawasiliano ya uhakika ili na wao watumie fursa hii kujitafutia kipato chao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, pale Chunya Mjini tuna changamoto kubwa sana ya mawasiliano hasa mnara wa Vodacom kiasi kwamba mawasiliano yamekuwa ni magumu na mtandao wa internet umekuwa ni changamoto kubwa sana.
Je, ni upi mpango wa Serikali sasa kushirikiana na kampuni ya Vodacom kuhakikisha kwamba unaongeza mnara wa mawasiliano pale Chunya Mjini ili mawasiliano yawe ya uhakika?

Name

Switbert Zacharia Mkama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kasaka kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninaanza kumpongeza kwa kuwa mfuatiliaji mzuri wa sekta hii ya mawasiliano. amekuwa akitufuatilia kwa karibu sana, Mheshimiwa Waziri na mimi, amekuwa akija Wizarani kufuatilia, kwa kweli anawapigania sana wananchi wa jimbo lake, hongera sana Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la kwanza la maeneo mengi kukosa mtandao hususan katika maeneo ya wachimbaji wadogo, ninapenda kumjulisha Mheshimiwa Mbunge kwamba kuna mradi tunaoutekeleza sasa hivi awamu ya 10 ambao tulisaini mkataba mwezi Disemba, 2025 na unategemea kukamilika mwezi Machi, 2027. Katika jimbo lake tutajenga minara minne kwenye Kata za Bwawani ambapo mtoa huduma Vodacom watajenga, Kata ya Lupa itajengwa na mto huduma Airtel, Kata ya Mamba Vodacom na Kata ya Mtanila atajenga Airtel.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya umuhimu wa sekta hii ya uchimbaji mdogo mdogo, ninamwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa UCSAF kupitia katika maeneo yote ambayo kuna wachimbaji wadogo wadogo kufanya tathmini, tuangalie tunaweza kufanya nini kama hatua ya dharura kuhakikisha kwamba katika maeneo haya ya wachimbaji wadogo wadogo ambayo ni muhimu katika uchumi wa nchi yetu, wanapata mawasiliano ya uhakika ili waweze kufanya kazi yao kwa uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili la changamoto ya mawasiliano katika Mji wa Chunya Mjini, ninamwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa TCRA kufanya tathmini katika Mji huo wa Chunya kuona kwamba huo mnara uliopo wa Vodacom una tatizo gani. Kama umeelemewa, basi waangalie uwezekano wa kuongezea nguvu ili mawasiliano yapatikane ya uhakika na kama kunahitajika kujenga mnara mwingine, basi taarifa hiyo iletwe Wizarani ili tuwaelekeze UCSAF kuanza mchakato wa kuangalia namna wanavyotatua tatizo hilo kwa kujenga mnara mwingine. Ninakushukuru.

Name

Mecktridis Fratern Mdaku

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Malinyi

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Kijiji cha Shoga ili kutatua changamoto ya mawasiliano ya simu?

Supplementary Question 2

MHE. MECKTRIDIS F. MDAKU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na changamoto kubwa sana ya mawasiliano katika maeneo ya Jimbo la Malinyi hususan katika Kata za Usangule, Mtimbira, Biro pamoja na Ngoeranga.

Je, ni lini Serikali itakwenda kujenga minara katika maeneo yao hayo ili wananchi waweze kupata huduma ya mawasiliano?

Name

Switbert Zacharia Mkama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara inatekeleza mpango wa miaka mitano wa ujenzi wa minara katika maeneo yote yenye changamoto ya minara hapa nchini. Kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mpango wetu huu, tutayafikia maeneo yote yenye changamoto ya umeme yakiwemo maeneo aliyoyataja hayo. Kwa hiyo, mpango wetu huu wa miaka mitano unakusudia kutatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya mawasiliano nchini kama sio kuyamaliza kabisa. Nakushukuru.

Name

Yannick Ikayo Ndoinyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Kijiji cha Shoga ili kutatua changamoto ya mawasiliano ya simu?

Supplementary Question 3

MHE. YANNICK I. NDOINYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni nini mpango wa Serikali wa kusambaza minara ya mawasiliano katika Kata za Wilaya ya Ngorongoro hasa zile ambazo ziko pembezoni mwa njia kuu? Ahsante sana.

Name

Switbert Zacharia Mkama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Ngorongoro, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa Serikali kusambaza minara nimewaeleza kwamba uko katika mpango wetu wa miaka mitano wa kuhakikisha kwamba tunatatua changamoto ya mawasiliano katika nchi hii, tunaitatua au tunaimaliza kabisa, na katika maeneo ya mpakani, tuna mradi wa awamu ya 11 ambao utajikita katika ujenzi wa minara katika maeneo ya mpakani, maeneo ya reli, maeneo ya SGR, MGR, TAZARA na maeneo maeneo yote ya kimkakati ya mpakani ambayo yote tutayajenga katika awamu ijao ya awamu ya 11 ambayo iko katika hatua ya manunuzi hivi sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwenye maeneo yote yenye changamoto, tutayashughulikia awamu ya 11 ambayo iko kwenye awamu ya ya manunuzi. Hatua ya manunuzi na mengine yatakayobaki tutayatekeleza katika mpango wetu wa miaka mitano wa ujenzi wa minara nchi nzima. Ninakushukuru.

Name

Florent Laurent Kyombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Kijiji cha Shoga ili kutatua changamoto ya mawasiliano ya simu?

Supplementary Question 4

MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninaipongeza Serikali imejenga minara kama mitano ndani ya Jimbo la Misenyi, lakini bado vijiji mbalimbali ndani ya Kata za Bugandika, Kitobo, Minziro na maeneo mengine bado tuna shida ya mtandao.

Je, ni lini sasa tutakamilisha ujenzi wa minara hiyo ili wananchi wote waweze kupata mawasiliano kwa sababu ya shughuli za kiuchumi?

Name

Switbert Zacharia Mkama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mbunge wa Misenyi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba changamoto ya mawasiliano katika jimbo lako tunaitambua na jimbo lako pia liko katika mpango wetu wa mkakati wa miaka mitano ya ujenzi wa minara. Kwa hiyo ninaomba tu tuendelee kuwa na subira, tutakuwa tunaijenga hii minara kwa awamu katika miaka hii mitano. Ifikapo mwaka 2030 tunaamini kwamba changamoto ya mawasiliano nchi nzima tutakuwa tumeitatua.

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Kijiji cha Shoga ili kutatua changamoto ya mawasiliano ya simu?

Supplementary Question 5

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa katika Jimbo la Kilolo kuna baadhi ya vijiji vya Kata ya Kimala, Masisiwe, Ibumu, Mlafu, Udekwa, Ruaha Mbuyuni, Nyanzwa, Mahenge, Ihimbo na Kijiji cha Kiwili, haya maeneo, vijiji hivi havina mawasiliano kabisa na bahati mbaya sana hata miundombinu ya barabara siyo mizuri. Je, Mheshimiwa Waziri upo tayari sasa kuja katika Jimbo la Kilolo ili uje uone wananchi wa vijiji hivi wanavyopata shida?

Name

Switbert Zacharia Mkama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nijibu swali la Mheshimiwa Ritta Kabati, Mbunge Kilolo kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Ritta kwamba niko tayari kuandamana naye kwenda katika jimbo lake kufanya tathmini na kujionea changamoto ya mawasiliano katika jimbo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kata alizozitaja, nimhakikishie kwamba tunalipa umuhimu mkubwa suala la mawasiliano nchini na ninapenda kumwelekeza kupitia Bunge lako Tukufu, Mkurugenzi Mkuu wa UCSAF kwenda katika Jimbo la Kilolo kufanya tathmini ya changamoto, amesema hakuna mawasiliano kabisa. Kwa hiyo, twende tufanye tathmini, tuone ni hatua gani za dharura tunaweza kufanya, lakini katika awamu ya 10, kuna mnara utajengwa katika Kata moja ya Mlafu na mnara mwingine utajengwa katika Kata ya Ukwega katika jimbo lake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kata nyingine zilizobaki ambazo amezitaja kata nane zilizobaki, ninamwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa UCSAF aende kulifanyia kazi suala hili mapema iwezekanavyo. Ninakushukuru.

Name

Fadhili Fabian Ngajilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Kijiji cha Shoga ili kutatua changamoto ya mawasiliano ya simu?

Supplementary Question 6

MHE. FADHILI F. NGALIJO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kwangu Jimbo la Iringa Mjini siyo kwamba tuna tatizo la minara, minara ipo, lakini haina nguvu. Kwa hiyo, ninaomba uangalie namna ya kufika kwenye maeneo ya ya Ugele, Msisina, Mtaragala, Kigonzile, Mkoga, Kitasengwa pamoja na eneo ambalo linaitwa Mosi, Mtaa wa Mosi liliopo Kata ya Kitwiru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali, je, Mheshimiwa Waziri unaweza sasa ukatuma wataalam wako wakaenda kufanya tathmini na kuhakikisha kwamba mawasiliano yanapatikana hasa eneo lile linalozunguka Uwanja wa Ndege wa Nduli ambao Mheshimiwa Dkt. Samia ameweka pale zaidi ya shilingi bilioni 63?

Name

Switbert Zacharia Mkama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Iringa Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawaelekeza na ninamwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa TCRA apeleke wataalam wake kufanya tathmini katika eneo hili la Iringa Mjini ili kujua chanzo cha tatizo hilo ni nini na kama ni kuongezea nguvu minara iliyopo ambayo amesema ipo, basi awasiliane na watoa huduma ili wakamilishe hiyo kazi. Nakushukuru.

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Kijiji cha Shoga ili kutatua changamoto ya mawasiliano ya simu?

Supplementary Question 7

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaishukuru sana Serikali kwa kunipa minara nane ya mawasiliano, lakini bado nina changamoto kwa kata ya Sirop pamoja na Kata ya Dawar hakuna kabisa minara ya mawasiliano. (Makofi)

Je, ni lini Serikali sasa itanipa katika kata hizi mbili minara ya mawasiliano kwa sababu hakuna mnara wowote pamoja na maeneo mengine ya Jimbo la Hanang yenye changamoto?

Name

Switbert Zacharia Mkama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Asia, Mbunge wa Hanang, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli katika awamu ya 10 hii tunajenga minara minane katika jimbo lake katika kata nane na bado kuna kata zina changamoto. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mpango wetu wa miaka mitano wa ujenzi wa minara na hizo kata tutazifikia.

Kwa hiyo, ninaomba aendelee kuvuta subira tukamilishe kwanza hii minara minane tunayoijenga halafu tuendelee kushughulikia na hizo kata zingine ambazo zina changamoto. Ninakushukuru.

Name

Joseph Zacharius Kamonga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ludewa

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Kijiji cha Shoga ili kutatua changamoto ya mawasiliano ya simu?

Supplementary Question 8

MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kule Ludewa Tarafa ya Mwambao ambayo ina kata zaidi ya tano kuna changamoto kubwa sana ya mawasiliano. Ninashukuru Serikali ilishaenda Makonde na Nsisi, hadi wananchi wameshatoa maeneo, lakini minara haijaanza kujengwa. Ni lini sasa wataalam watakwenda kwa ajili ya ujenzi wa minara hiyo? Ahsante.

Name

Switbert Zacharia Mkama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Kamonga, Mbunge wa Ludewa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamwelekeze tu Mkurugenzi Mkuu wa UCSAF aende kule Ludewa kufanya tathmini ya changamoto ya mawasiliano iliyopo na kuchukua hatua zinazostahili. Ninakushukuru.

Name

Christina Solomon Mndeme

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Kijiji cha Shoga ili kutatua changamoto ya mawasiliano ya simu?

Supplementary Question 9

MHE. CHRISTINA S. MNDEME: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwa kuwa Serikali imekuwa ikiendelea kuwafikishia wananchi mawasiliano ya simu ikiwemo kuwajengea minara, tunaipongeza sana Serikali; na kwa kuwa pamoja na juhudi nzuri za Serikali, lakini bado maeneo mengine ndani ya Mkoa wa Tabora hayana mawasiliano ya simu.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapelekea mawasiliano wananchi wa Kata za Igulungu, Makazi, Kijiji cha Katunda, Kata ya Mabama, Kata ya Ibili, Wilaya ya Uyui, Kata za Nhwande, Kata ya Igwisi, Kata ya Ukumbi Siganga, Kata ya Ugunga, Wilaya ya Kaliua na Kata za kabila, Ikomwa, Kakola, Mtalikwa na Ndevelwa Kijiji cha Ng'ombe zilizopo Manispaa ya Tabora? Ahsante.

Name

Switbert Zacharia Mkama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali Mheshimiwa Mndeme, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizo kata zote alizozitaja tumeziingiza katika mpango wetu wa miaka mitano wa ujenzi wa minara nchi nzima. Kwa hiyo, katika kipindi hiki cha miaka hii mitano, kata zote hizo tutazifikia pamoja na kata zote za Waheshimiwa Wabunge waliomo katika Bunge lako Tukufu kote nchini. Ninakushukuru.

Name

Esther Lukago Midimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Kijiji cha Shoga ili kutatua changamoto ya mawasiliano ya simu?

Supplementary Question 10

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kijiji cha Kijirishi, Kata ya Mkula Wilaya ya Busega hakina mawasiliano kabisa. Ni lini Serikali itajenga mnara wa mawasiliano katika kijiji hicho?

Name

Switbert Zacharia Mkama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hivyo kijiji alichokitaja na chenyewe tumekihusisha katika mpango wetu wa miaka mitano wa ujenzi wa minara nchi hii. Kwa hiyo, katika kipindi hiki cha miaka hii mitano tutavifikia vijiji vyote awamu kwa awamu, hatua kwa hatua na kuhakikisha kwamba tutakapofika mwaka 2030 kila eneo lenye changamoto ya mawasiliano nchini tutakuwa tumelifikia. Nakushukuru.

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Kijiji cha Shoga ili kutatua changamoto ya mawasiliano ya simu?

Supplementary Question 11

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, unaweza ukaona kwamba idadi ya Wabunge wanaoomba minara ni wengi na Serikali kwa nyakati tofauti mmekuwa mkionyeshwa kwamba mna interest ya kufunga satellite ili tuachane na biashara ya minara. Upi mkakato wa Serikali na umefikia hatua ipi kwenye ujenzi wa kupatikana kwa satellite nchini ili mawasiliano yapatikane nchi nzima?

Name

Switbert Zacharia Mkama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Sanga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mpango wa Serikali kupata satellite, mpango huu tunaendelea nao na katika mwaka ujao wa fedha katika hii bajeti mliyotupitishia mpango huu tutautekeleza. Ninakushukuru.

Name

Fadhili Ally Liwaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nachingwea

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Kijiji cha Shoga ili kutatua changamoto ya mawasiliano ya simu?

Supplementary Question 12

MHE. FADHILI A. LIWAKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru, wananchi wa Kilimarondo na Kiegei wanatembea umbali wa kilometa 126 kufuata huduma ya kifedha inayotokana na mitandao ya simu. Je, Serikali ina mkakati gani kuwajengea minara ya uhakika ili kupata huduma hiyo?

Name

Switbert Zacharia Mkama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nijibu swali la Mheshimiwa Fadhili Liwaka kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo hayo aliyoyataja kama nilivyoeleza awali yote yako katika mpango mkakati wa Serikali wa Miaka Mitano wa Ujenzi wa Minara katika maeneo yote yenye changamoto hapa nchini.

Kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Fadhili kwamba maeneo yote aliyoyataja hayo tutayafikia katika kipindi hiki cha mkakati huu kwa sababu tunakwenda hatua kwa hatua kulingana na upatikanaji wa fedha. Kwa hiyo, kadri fedha inavyopatikana, tutakuwa tunatekeleza mkakati wetu na tunategemea kwamba ifikapo mwaka 2030 changamoto ya mawasiliano nchini itakuwa tumeitatua au tumeimaliza kabisa.