Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 27 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 308 | 2026-05-12 |
Name
Charles Mhando Njama
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Korogwe Mjini
Primary Question
MHE. CHARLES M. NJAMA aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa vituo vya afya Kata ya Old Korogwe, Kwamndolwa, Mtonga na Bagamoyo utaanza?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA
SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Charles Mhando Njama, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini, kama
ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Old Korogwe ina jumla ya wakazi 8,126 ambao wanapata huduma za upasuaji katika Kituo cha Afya Majengo. Kata ya Kwamndolwa ina wakazi 5,354, wakazi wa Kata hiyo wanapata huduma kwenye Hospitali ya Magunga iliyopo kilometa 15. Kata ya Bagamoyo ina wakazi 7,945, huduma za upasuaji
wanazipata kwenye Hospitali ya Magunga iliyopo kilometa 10.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Mtonga ina wakazi 16,300, huduma za upasuaji wanazipata kwenye Hospitali ya Magunga iliyopo kilometa 18. Kata ya Mtonga ina uhitaji zaidi ambapo ina wananchi 16,300 na wanapata huduma ya upasuaji katika hospitali ya Wilaya, umbali wa kilometa 18. Serikali itaweka mpango wa ujenzi wa kituo cha afya katika Kata ya Mtonga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeweka kipaumbele cha kukamilisha miradi viporo ya huduma za afya katika vituo vya afya 364, ili viweze kutoa huduma stahiki, zikiwemo huduma za dharura za
upasuaji, ambapo mwaka 2026/2027 jumla ya vituo 111 vimetengewa
shilingi bilioni 23.37, kwa ajili ya kuongezea miundombinu muhimu.
Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya
kwenye Kata za kimkakati zitakazokidhi vigezo katika Halmashauri ya
Mji wa Korogwe, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved