Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Charles Mhando Njama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Primary Question

MHE. CHARLES M. NJAMA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa vituo vya afya Kata ya Old Korogwe, Kwamndolwa, Mtonga na Bagamoyo utaanza?

Supplementary Question 1

MHE. CHARLES M. NJAMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, ninamshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ambayo ametupatia, lakini nina maswali mengine mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza. Kama ulivyoeleza katika majibu yako, Kituo chetu cha Afya cha Kata ya Majengo kinahudumia wananchi wengi zaidi, siyo tu wa Kata ya Majengo, kulingana na maeneo kilipo, kinahudumia watu wengi wa eneo la
Jimbo la Korogwe Mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepata shilingi 500,000,000 ambazo zimetusaidia kuboresha sana kituo kile cha afya na sasa kimekuwa kikihudumia takribani wananchi 2,200 kwa mwezi, ambapo kinakaribia Hospitali yetu ya Magunga, lakini kituo kile kina changamoto kubwa ya OPD. Je, ni lini Serikali itakuwa tayari kutenga fedha, kwa ajili ya kwenda kuboresha OPD ya Kituo chetu cha Afya cha Majengo, ili wananchi waweze kupata huduma nzuri zaidi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili. Tuna vituo vitatu vya afya, Majengo, Mgombezi pamoja na Kwa Msisi, lakini havina ambulance. Je, Serikali iko tayari kuwaambia wananchi wa Korogwe Mjini, ni lini vituo hivi vya afya vitapa ambulance ili kurahisisha huduma pale ambapo tunapata hali ya dharura, hasa kwa akina mama
wajawazito? Ahsante sana.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, ninampongeza sana Mheshimiwa Charles Mhando Njama, Mbunge wa Korogwe Mjini, amewasilisha hoja hii kwa niaba ya wananchi wa Korogwe Mjini mara kadhaa. Serikali hii sikivu ya Awamu ya Sita imechukua hoja zote za Mheshimiwa Mbunge, kwa
ajili ya kuhakikisha kwamba, tunaboresha huduma za afya katika Jimbo la Korogwe Mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu kwamba, fedha
iliyopelekwa Kituo cha Afya cha Majengo ambacho kinahudumia wananchi wengi imefanya kazi nzuri, lakini bado tuna upungufu wa baadhi ya miundombinu ikiwemo Jengo la OPD. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, ujenzi wa vituo hivi vya afya ni endelevu. Tulianza na awamu ya kwanza, tumejenga majengo yaliyopo sasa, lakini tutakwenda na awamu ya pili, kwa ajili ya kuhakikisha tunajenga majengo yanayopungua katika vituo hivyo, ili kuviwezesha kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, tunafahamu kwamba, vituo vya afya vinahitaji magari ya wagonjwa, kwa maana ya ambulance. Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita Serikali imepeleka ambulance kwenye vituo vya afya na hospitali za wilaya katika Mamlaka za
Serikali za Mitaa, zaidi ya magari ya wagonjwa 500 na Serikali inaendelea kutenga fedha kwa awamu kupeleka magari ya wagonjwa kwenye Vituo vya Afya ikiwemo Kwa Msisi, Majengo na vituo vingine ambavyo vitahitaji magari ya wagonjwa. (Makofi)

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CHARLES M. NJAMA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa vituo vya afya Kata ya Old Korogwe, Kwamndolwa, Mtonga na Bagamoyo utaanza?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa, Kata ya Didia ambayo iko Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ni ya kimkakati, ina idadi kubwa ya watu na ni kata ambayo inazalisha sana zao la mpunga. Je, ni lini Serikali itajenga kituo cha afya katika kata hii?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ninampongeza sana dada yangu, Mheshimiwa Dkt. Christina Mnzava, amekuwa mfuatiliaji wa karibu
kuhusiana na ujenzi wa kituo cha afya kwenye kata hiyo ya kimkakati katika Wilaya ya Shinyanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali inaendelea kufanya tathmini na kuainisha kata zenye idadi kubwa ya wananchi, ambazo ziko umbali mrefu kutoka vituo vya karibu kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya.
Tutahakikisha tumetoa kipaumbele katika kata hiyo, ili kwa awamu tuendelee kupeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya kila kata.

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CHARLES M. NJAMA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa vituo vya afya Kata ya Old Korogwe, Kwamndolwa, Mtonga na Bagamoyo utaanza?

Supplementary Question 3

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Ninazipongeza jitihada za Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan toka ameingia madarakani tumepata vituo vya afya karibu vinne, lakini Jimbo la
Hanang lina upungufu wa vituo vya afya 24. Je, ni lini Serikali itatuongezea vituo vya afya kwa sababu, bado tuna uhitaji mkubwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa vile ambavyo vimekamilika kwa jitihada ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni lini sasa tutapewa vifaatiba ili tuweze kupata huduma? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa vituo vya afya ni zoezi endelevu na ni kweli kama Mheshimiwa Asia Halamga, Mbunge wa Hanang, alivyosema. Serikali tutapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya katika Jimbo la Hanang.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakuhakikishia Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Hanang, tunaendelea kufanya tathmini na kuainisha kata za kimkakati zenye vigezo na kuendelea kutenga fedha kwa awamu, ili tuendelee kusogeza huduma za afya, lakini pia, vifaa tiba katika vituo vyetu ambavyo tunajenga katika Jimbo la Hanang na katika maeneo yote kote nchini. (Makofi)

Name

Mariam Nassoro Kisangi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Temeke

Primary Question

MHE. CHARLES M. NJAMA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa vituo vya afya Kata ya Old Korogwe, Kwamndolwa, Mtonga na Bagamoyo utaanza?

Supplementary Question 4

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi niulize swali la nyongeza. Kata ya Sandali katika Jimbo la Temeke ina wakazi wanaokaribia 40,000 na zaidi, lakini hakuna kituo cha afya. Je, Serikali lini itajenga kituo cha afya katika Kata ya Sandali iliyopo katika Jimbo la Temeke? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ziko kata ambazo zina idadi kubwa sana ya wananchi na
maelekezo ya Serikali yametolewa kwa Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na hususan halmashauri zile ambazo angalau zina mapato makubwa ya ndani, kama Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natumia nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, kuwakumbusha Wakurugenzi, kumkumbusha Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke na kumsisitiza
kwamba, ni muhimu kufanya tathmini. Ikiwa kata hiyo inahitaji kujenga kituo cha afya kwa idadi ya wananchi waliopo na umbali kutoka kituo kingine, basi hatua za kutenga fedha za mapato ya ndani zianze na ujenzi uanze wakati Serikali kuu pia inatafuta fedha kwenda
kuwaunga mkono na kukamilisha vituo hivyo vya afya.