Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 27 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 309 2026-05-12

Name

Yohana Stephen Msita

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Itigi

Primary Question

MHE. YOHANA S. MSITA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Vituo vya Afya Kata za Mgandu, Mwamagembe, Ipole na Idodyandole – Itigi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA
SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Yohana Stephen Msita, Mbunge wa Jimbo la Itigi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha miaka mitano, Halmashauri ya Wilaya ya Itigi imepokea jumla ya shilingi bilioni 3.34
kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Halmashauri kwa shilingi bilioni 1.75,
ujenzi wa vituo vya afya viwili shilingi bilioni 1.186 na ukamilishaji wa
maboma ya zahanati 11 shilingi 650,000,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imetoa shilingi 686,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Idodyandole, ujenzi unaendelea. Aidha, katika mwaka wa fedha
2026/2027 Serikali imetenga shilingi 800,000,000 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa miundombinu katika Hospitali ya Wilaya ya Itigi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea na ujenzi wa vituo vya afya katika Kata za kimkakati, zikiwemo Kata za Mwamagembe,
Mgandu na Ipole kwa kuzingatia vigezo na upatikanaji wa fedha,
ahsante.