Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Yohana Stephen Msita

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Itigi

Primary Question

MHE. YOHANA S. MSITA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Vituo vya Afya Kata za Mgandu, Mwamagembe, Ipole na Idodyandole – Itigi?

Supplementary Question 1

MHE. YOHANA S. MSITA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, wananchi wa Itigi
wamekuwa wakijitolea kwa nguvu na mali zao katika kujenga majengo ya vituo vya afya na zahanati kama maeneo ya Mkajenga, Agondi, Matumaini na Itagata, je, Serikali haioni sasa umuhimu wa kuharakisha utoaji wa fedha ili waendelee kuwasaidia wananchi hawa katika juhudi ambazo wanaendelea kuzionesha?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, Serikali ina mpango gani wa kujenga jengo la X-Ray katika Kituo cha Afya pale Itigi pamoja na kupeleka X-Ray machine? Ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, ninampongeza sana sana Mheshimiwa Yohana
Stephen Msita, Mbunge wa Itigi na wananchi wa Itigi kwa kuendelea kutoa nguvu zao na michango yao mbalimbali katika kuibua miradi ya ujenzi wa zahanati na vituo vya afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ni mwongozo wa Serikali, na Serikali siku zote imekuwa ikitenga fedha kwenda kuwaunga mkono wananchi kwenye umaliziaji wa maboma ya zahanati. Katika miaka mitano iliyopita, fedha nyingi zimetolewa kwa ajili ya kukamilisha maboma ya zahanati. Serikali itaendelea kutenga fedha kwenye bajeti zake kwenda kuwaunga mkono wananchi ambao wameanza ujenzi wa zahanati kwa nguvu zao katika maeneo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Msita kwamba tutahakikisha pia tunatoa kipaumbele kwenye maboma ambayo yameanzishwa na wananchi katika Jimbo la Itigi katika ukamilishaji wa zahanati hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, tunafahamu katika vituo vyetu vya afya ni muhimu kuwa na majengo ya X-Ray, lakini pia na mashine zenyewe za X-Ray. Serikali imeendelea kujenga majengo ya X-Ray kwa awamu na tutaendelea pia kupeleka mashine hizi ili kuboresha
vipimo katika vituo vya afya kikiwemo kituo hicho cha afya ambacho Mheshimiwa Mbunge amekitaja.

Name

Zuberi Yahya Mfaume

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini

Primary Question

MHE. YOHANA S. MSITA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Vituo vya Afya Kata za Mgandu, Mwamagembe, Ipole na Idodyandole – Itigi?

Supplementary Question 2

MHE. ZUBERI Y. MFAUME: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Kwanza, niipongeze Serikali kwa kasi ya kujenga vituo vya afya nchi nzima. Pia, nina swali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Kibogwa iliyopo katika Jimbo la Morogoro Kusini ni kata iliyoko milimani na ina mito mikubwa ya kuvuka na wanapaswa kusafiri umbali wa kilomita 50 kufikia vituo vya afya. Je, Serikali ina mpango gani sasa kupeleka kituo cha afya katika Kata ya Kibogwa? Ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ilishaweka mpango mkakati wa kuainisha maeneo
ambayo yana idadi kubwa ya wananchi na Kata ambazo ziko maeneo ya mbali zaidi kutoka kituo cha karibu kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge anasema, kilomita 50, na pia hali ya kijiografia ya maeneo husika kama visiwa, milimani na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo haya kwa kawaida yanapewa kipaumbele zaidi kujenga vituo vya afya ili kusogeza huduma karibu na wananchi. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tumepokea hoja hiyo, tutafanya mawasiliano na Halmashauri ya
Morogoro ili kuweza kuona kama Kata hiyo inakidhi vigezo tuanze kuiweka kwenye mipango yetu ya mapato ya ndani ya halmashauri na Serikali Kuu kwa ajili ya kuendelea kutenga fedha kwa awamu kwa
ujenzi wa kituo cha afya.

Name

Edefonce Joackim Canoni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Primary Question

MHE. YOHANA S. MSITA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Vituo vya Afya Kata za Mgandu, Mwamagembe, Ipole na Idodyandole – Itigi?

Supplementary Question 3

MHE. EDIFONSI J. KANONI: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali la nyongeza. Jimbo la Kalambo katika Kijiji cha Msishindwe, Tiangoma, Rolesha, Mpombwe, Nondo, Musoma, Kafukoka, Mikonko, Kalembe, Panga, Kiundilamema, Kitwanga, Mnamba pamoja Tunyi ni vijiji ambavyo wananchi wamejenga vituo vya afya kufikia usawa wa lenta. Ni nini mpango wa Serikali wa kutenga bajeti kwa ajili ya kukamilisha hizo zahanati ili wananchi waandelee kunufaika na huduma ya afya? Ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mheshimiwa Kanoni alishawasilisha orodha
ya maboma ya zahanati ambayo yanahitaji umaliziaji. Nitumie nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Kalambo kwa kutoa michango yao na kuanza ujenzi wa maboma ya
zahanati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie tu kwamba tutaendelea kutenga fedha kwa awamu kuwaunga mkono wananchi katika juhudi zao kukamilisha maboma ili kuanza kutoa huduma katika
vijiji ambavyo amevitaja ambavyo tayari vina maboma ya zahanati.

Name

Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba kusini

Primary Question

MHE. YOHANA S. MSITA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Vituo vya Afya Kata za Mgandu, Mwamagembe, Ipole na Idodyandole – Itigi?

Supplementary Question 4

MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana. Kijiji cha Kisana kuna zahanati ambayo imejengwa zaidi ya miaka 12 iliyopita katika Kata ya Kyebitembe katika Jimbo la
Muleba Kusini. Je, Serikali ina mkakati gani kumaliza maboma ambayo yana miaka zaidi ya 10 bila kutumika na wananchi walitoa nguvu zao katika ujenzi wa maboma hayo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ilipeleka
zaidi ya shilingi 25,000,000,000 kwenye Halmashauri na Majimbo yetu kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi. Kigezo ambacho kilikuwa kinatumika kimojawapo kilikuwa
ni maboma yale ambayo yamejengwa muda mrefu zaidi kupewa kipaumbele kupelekewa fedha kukamilika na kuanza kutoa huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Kikoyo kwamba maboma hayo ambayo yana muda mrefu, bado yako kwenye mpango Serikali na Serikali inaendelea na taratibu za kibajeti na kupeleka fedha kwa ajili ya ukamilishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nitoe wito kwa Halmashauri kwa yale maboma ambayo yamekaa muda mrefu na yako ndani ya uwezo wa mapato ya ndani ya halmashauri waendelee pia kutenga fedha kwa awamu kila mwaka wa fedha kwa ajili ya ukamilishaji ili kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.

Name

Esther Nicholas Matiko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Tarime Mjini

Primary Question

MHE. YOHANA S. MSITA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Vituo vya Afya Kata za Mgandu, Mwamagembe, Ipole na Idodyandole – Itigi?

Supplementary Question 5

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kata ya Kenyamanyori ni Kata iko nje ya Mji wa Tarime na wananchi wanapata adha kubwa sana kuja kupata huduma kwenye Hospitali ya Mji wa Tarime na miundombinu ya barabara siyo rafiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, wananchi wameshaanza kujenga kituo cha afya na hata Mfuko wa Jimbo tulipeleka fedha pale, Serikali inaweka juhudi gani za dharura kuhakikisha kwamba inapeleka fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa kituo cha afya kwenye Kata ya Kenyamanyori?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawapongeza sana wananchi wa Jimbo la Tarime Mjini na Mbunge wa Jimbo hili, Mheshimiwa dada Esther Matiko kwa kuhamasisha wananchi kuanza ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo ambayo ipo pembezoni na mbali kutoka vituo vya afya vya jirani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tumepokea hoja hiyo, lakini nitumie nafasi hii pia kumsisitiza Mkurugenzi kuona uwezekano wa kuanza kutenga fedha angalau kidogo kwa mapato ya ndani wakati sisi Serikali Kuu tunaendelea na kuandaa fedha kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa vituo hivyo vya afya.