Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 27 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 310 | 2026-05-12 |
Name
Haiderali Hussein Gulamali
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ilongero
Primary Question
MHE. HAIDERALI H. GULAMALI aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Soko la Vitunguu Njia panda ya Merya?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Haiderali Hussein Gulamali, Mbunge wa Jimbo la Ilongero, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua uhitaji wa soko la vitunguu katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Kutokana na uhitaji huo, Halmashauri iliandaa andiko mradi lenye thamani ya shilingi bilioni 2.9. Mwezi Septemba, 2024 Halmashauri ya Wilaya ya Singida iliwasilisha andiko Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kuomba ushirikiano katika utekelezaji wa mradi huu. Wizara ya Kilimo iliridhia ombi hilo ambapo ujenzi wa soko hili utafanyika kwa ushirikiano kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Singida na Wizara ya Kilimo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua iliyofikiwa kwa sasa ni kuandaa mkataba wa makubaliano kuhusu namna mradi utavyotekelezwa na pande zote mbili. Mara baada ya makubaliano hayo kukamilika, taratibu za ujenzi zitaanza rasmi, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved