Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Lucy Thomas Mayenga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAIDERALI H. GULAMALI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Soko la Vitunguu Njia panda ya Merya?
Supplementary Question 1
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Songwa ina akina mama ambao ni wachapakazi sana ambao wamejituma kwa muda mrefu kulima kilimo cha nyanya. Je, ni lini Serikali na hasa Mheshimiwa Naibu Waziri atakuja Kata ile ya Songwa kipindi cha msimu aone jinsi akina mama wale chini ya Diwani wao Mheshimiwa Ngolomole wanavyohangaika na masoko ili aweze kufikiria kujenga soko la nyanya katika eneo hilo?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sana dada yangu Mheshimiwa Lucy Mayenga, Mbunge wa Jimbo la Kishapu. Ninakumbuka suala hili alishaliwasilisha Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, na sisi tumeendelea kuwasiliana na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kuanza kuandaa michoro na makadirio ya gharama ili kuanza kutenga fedha ya mapato ya ndani wakati tunasubiri fedha za kutoka Serikali Kuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba moja ya vipaumbele vya Serikali ni kuboresha maeneo ya kufanyia biashara ya wajasiriamali wodogo wadogo ili kuhakikisha kwamba wanastawi kiuchumi na tutahakikisha kwamba tunaendelea kufanya hivyo katika maeneo yote likiwemo Jimbo la Kishapu.
Name
Emmanuel John Khambay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Mjini
Primary Question
MHE. HAIDERALI H. GULAMALI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Soko la Vitunguu Njia panda ya Merya?
Supplementary Question 2
MHE. EMMANUEL J. KHAMBAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Mji wa Babati ni mji ambao unakua kwa kasi. Je, ni lini Serikali itatoa shilingi 5,000,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Babati?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mji wa Babati ni moja ya mji ambao iko kwenye mradi wa TACTIC wa Miji 45 na ninafahamu kuna miundombinu kadhaa ambayo inatarajiwa kujengwa katika Mji wa Babati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Khambay, Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, kwamba Serikali iko kwenye hatua nzuri za kutekeleza miradi hiyo kuhakikisha kwamba tunajenga masoko, barabara lakini na miundombinu mingine ili Mji wetu wa Babati uendelee kuwa Mji wa kisasa na bora zaidi kwa maslahi ya wananchi.
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Primary Question
MHE. HAIDERALI H. GULAMALI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Soko la Vitunguu Njia panda ya Merya?
Supplementary Question 3
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Kuna masoko madogo madogo ya Halmashauri zetu ambapo Halmashauri zinakusanya kodi, lakini hakuna vyoo katika maeneo hayo hali inayopelekea kuchafua mazingira. Serikali inaweza ikatoa agizo kwa Wakurugenzi nchi nzima, kila palipo na mkusanyiko wa kufanyia biashara na wanakusanya kodi wachimbe vyoo na kuweka maji ili kutimiza usafi? Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ni wajibu wa Halmashauri zetu yale maeneo yote ambayo yana masoko ni lazima yawe na miundombinu yote muhimu ya kiafya na huduma za kijamii katika maeneo hayo. Mojawapo ni kuwa na vyoo, maji na miundombinu mingine muhimu ya msingi na wezeshi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, kuwasisitiza Wakurugenzi wote kwamba ni lazima kila soko ambalo lina mkusanyiko wa wananchi wahakikishe miundombinu ya vyoo ipo, maji yanapatikana na ule ushuru ambao wanaukusanya katika maeneo hayo iwe ni sehemu ya fedha inayorejea kuboresha miundombinu ile ili wananchi waweze kufanya kazi katika mazingira bora, lakini pia kuepusha uwezekano wa milipuko ya magonjwa katika maeneo ya masoko.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved