Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 27 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 311 2026-05-12

Name

Dr. Wilson Charles Mahera

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Primary Question

MHE. DKT. WILSON C. MAHERA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza na kukamilisha utekelezaji wa ujenzi na ukarabati wa barabara katika Jimbo la Butiama?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Wilson Mahera Charles, Mbunge wa Jimbo la Butiama, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya aya Butiama ina mtandao wa barabara wa kilometa 596.62 unaohudumiwa na Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini. Serikali imekuwa ikitenga bajeti ya matengenezo, ukarabati na ujenzi wa barabara mbalimbali ambapo bajeti ya Wilaya imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Wilaya ya Butiama limeidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 2.59 kwa ajili ya matengenezo na ukarabati wa barabara maeneo korofi yenye urefu wa Kilometa 145.32 na ujenzi wa madaraja 14 pamoja na makalavati 26. Kazi hizi baadhi yake zinaendelea kutekelezwa maeneo mbalimbali ya Jimbo la Butiama ambapo kiasi cha shilingi 722,649,050 kimepelekwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 2.74 kwa ajili ya Wilaya ya Butiama kwa ajili ya matengenezo na ukarabati wa barabara maeneo korofi yenye urefu wa Kilometa 155.42 na ujenzi wa madaraja 17 na makalavati 29.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi na ukarabati wa barabara za wilaya ya Butiama ili kuwawezesha wananchi kuendelea na shughuli za kiuchumi, ahsante.